Blog.

RadioOne - 2025-12-22T03:00:00.628Z

RadioOne

--:--
--:--

Transcription

Radio one inakuletea kipindi cha bbc.

Ni 10:02 saa za Afrika Mashariki sawa na 11:00 Afrika ya kati hujambo mimi ni martha saranga karibu katika amka na bbc kutoka idhaa ya Kiswahili ya bbc katika amka na bbc asubuhi hii maafisa nchini Marekani wanasema walinzi wa Pwani wanafuatilia meli nyingine ya mafuta nje ya Pwani ya Venezuela mateka 130 waliochukuliwa katika 1 ya matukio mabaya zaidi ya utekaji nchini Nigeria.

Waachiliwa huru na hii leo utasikia mfululizo wa makala maalum.

Za mwisho wa mwaka ambapo leo tunaangazia hali ya demokrasia Afrika Mashariki la barani Afrika kama ilivyoshuhudiwa katika kipindi cha mwaka huu 2025 activist wanapoingia katika nchi bora hawajakuja kupanga maandamano na kuhamasisha wananchi kwa chochote ama kufanya kazi yoyote kuleta hakuna matatizo yoyote wakiingia nchini kuja kushuhudia.

Yeah.

Naam na kwanza ni muhtasari wa habari za dunia bunge la New South Wales nchini Australia linajadili mageuzi ya umiliki wa silaha kufuatia ufyatuaji risasi uliolenga halaiki katika sherehe ya Wayahudi katika ufuo wa bundi wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu 10 na watano.

Mapendekezo hayo ambayo yanatarajiwa kupitishwa yanajumuisha masharti ya idadi ya silaha ambazo mtu anaweza kumiliki kwa upande wa wadau wanaotetea haki ya kumiliki silaha nchini humo, wanasema sheria hiyo imeharakishwa na itawaadhibu isivyo haki wamiliki wa silaha.

Tena Jumapili waziri mkuu wa Australia alizulumiwa katika sherehe ya kuwakumbuka waathiriwa serikali inashutumiwa kwa kutochukua hatua za kutosha kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi Kanisa pekee la Kikatoliki katika jiji la gaza limefanya ibada ya kwanza kuadhimisha sherehe za Krismasi ibada hiyo iliongozwa na kardinali pierbattista pizzaballa, kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Israel na katika maeneo ya Palestina ambaye amesema jumuiya hiyo inaendelea kuishi katika nyakati za giza na changamoto kubwa.

Kanisa la parokia ya familia takatifu lilipambwa kwa mapambo ya Krismasi wakati kardinali pizzaballa alipowasili hii ni ziara yake ya kwanza kuingia mjini gaza tangu kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi Oktoba kati ya Israel na hamas.

Mamlaka nchini Nigeria zinasema kuwa mateka 130 waliotekwa katika 1 ya matukio mabaya zaidi ya utekaji nchini humo wameachiliwa huru watu wenye silaha waliwakamata wanafunzi na wafanyakazi kutoka shule ya Kikatoliki katika jimbo la niger mwezi uliopita.

Serikali ya Nigeria inasema mateka wote 230 sasa wako huru, lakini polisi wanasema hesabu kamili ya watu bado haijakamilika bado haijafahamika ikiwa kuna malipo yoyote yaliyofanyika kufanikisha.

Kuachiliwa kwao.

Na mjumbe maalum wa rais wa Marekani Donald Trump katika mzozo wa Ukraine na urusi ameelezea siku 3 za mazungumzo huko miami zinazolenga kukomesha vita nchini Ukraine kama zenye tija na zenye kujenga akiandika kwenye mitandao ya kijamii.

Steve with of amesema kwamba Ukraine na urusi zilijitolea kikamilifu kukomesha vita wajumbe wanaohusika na mazungumzo hayo ikiwemo Marekani walikutana na pande zote 2 zinazohusika na mzozo unaoendelea.

Baadhi ya mazungumzo yaliyohusisha wajumbe wa Ukraine likiwemo wawakilishi kutoka kwa washirika kadhaa wa Umoja wa ulaya, jitihada za kidiplomasia zinafuatia shinikizo jipya.

Ambapo kwa rais trump na suluhisho la mgogoro huu unaokaribia miaka minne sasa.

Hii ni bbc.

Unaendelea kusikiliza amka na bbc kutoka idhaa ya Kiswahili ya bbc ikikutangazia kwenye fm radio washirika na Intanet katika bbc swahilidot.com ukiwa nchini Kenya unatupatia unatupata kupitia most fm Uganda ni voice of muhabura Tanzania unatupata kupitia cgfm visiwani Zanzibar ni zenji fm na iwapo upo nchini drc ya terehe sikio kupitia hali za dili redio.

Aidha unaweza kutufuatilia 1 kwa 1 kupitia ukurasa wetu wa Facebook wa bbc Swahili.

Tukaweka maoni yako hapo na tukipata wasaa tutasoma.

Mimi ni martha saranga maafisa nchini Marekani wanasema walinzi wa Pwani wanafuatilia meli nyingine ya mafuta katika maji ya kimataifa nje ya Pwani ya Venezuela.

Hii ni operesheni ya pili kufanyika wikendi hii mwishoni mwa juma Venezuela iliishutumu Marekani kwa uharamia wa kimataifa na utekaji nyara baada ya vikosi vyake kukamata meli ya mafuta huko karibian.

Maafisa wa Marekani wamesema meli hiyo ilikuwa imebeba mafuta yaliyotumika kufadhili kile walichokiita.

Ugaidi wanako lakini hawakutoa ushahidi wowote awali rais Donald Trump aliamuru kuzuiwa kwa mafuta kuingia na kutoka Venezuela.

Naye waziri wa mambo ya nje wa Marekani, marco rubio amezungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa juma lililopita akisema ni wazi kwamba Marekani haiwezi kuvumilia hali ya sasa na utawala wa Venezuela.

Principle behind msingi wa sera yetu ya mambo ya juzi siku linda maslahi ya taifa hivyo ni lazima kwanza yafunguliwe maslahi hayo tuitishe yatekelezwe tumebainisha kuwa tunaunga mkono sera za nyingine.

Only.

Ikiwezekana yote matano angalau mojawapo hii pia linahitaji kuweka vipaumbele kwa kuwa hata taifa lenye rasilimali nyingi zina mipaka ya muda rasilimali hiki.

Pia vikwazo vimewekwa kwa baadhi ya jamaa wa rais maduro na kwa biashara zinazohusiana na kile Marekani inachokiita utawala wake usio halali.

Mamlaka nchini Nigeria zimearifu kuwa waathiriwa 130 wa 1 kati ya utekaji nyara mkubwa zaidi kushuhudiwa nchini humo wameachiliwa huru washambuliaji waliojihami kwa silaha waliwataka watoto na wafanyakazi kutoka katika shule ya Kikatoliki iliyoko jimbo la niger mwezi uliopita.

Serikali inasema kuwa wanafunzi wote mia na 30 waliotekwa sasa wako huru lakini polisi wanasema wanaendelea na zoezi la uhakiki ambao bado haujakamilika sabatini zina taarifa zaidi mmiliki wa shule hiyo na mwenyekiti wa chama cha Wakristo nchini Nigeria.

CA katika jimbo la niger askofu buruse dawa yohana amethibitisha taarifa hiyo kwa bbc haijafahamika ikiwa kuna malipo yoyote yaliyofanyika ili kuwezesha kuachiliwa kwa mateka hao siku ya jana Jumapili.

Msemaji wa rais sunday dare alitangaza kupitia akaunti yake rasmi ya mtandao wa x kwamba hakuna mwanafunzi wale wafanyakazi wa shule aliyesalia mikononi mwa watekaji nyara.

Kamishna wa polisi wa jimbo la niger, adam abdullahi elman ameiambia bbc kuwa kundi la mwisho la walioachiliwa huru.

Limeendelea kufanyiwa uhakiki na vikosi vya usalama na kwamba watapelekwa shuleni leo siku ya Jumatatu ili kuwaonesha tena na familia zao walioachiliwa huru ni wanafunzi 303 na walimu 12 waliotekwa kutoka katika shule ya Kikatoliki iseti marys baada ya watu wenye silaha kuvamia bweni la shule hiyo alfajiri ya 11/21.

Uongozi wa shule umeeleza kuwa wanafunzi 50 walitoroka wakati wa shambulio hilo hali iliyosababisha zaidi ya wanafunzi 200 kujikuta mikononi mwa watekaji tarehe 8 Desemba.

Mamlaka ziliokoa wanafunzi 99 na mwalimu mmoja huku wengine takriban 160 na watano wakiendelea kushikiliwa.

Hata hivyo, kamishna wa polisi wa jimbo la niger ameieleza bbc kuwa watu 130 waliokombolewa hivi karibuni wanakamilisha idadi ya waliokuwa wamesalia akieleza kuwa takwimu za awali zilizotolewa na uongozi wa shule hazikuwa sahihi kufuatia visa vya utekaji wa mara kwa mara katika majimbo ya niger na kelly mwezi Novemba, serikali ya Nigeria ilitangaza kuzifunga shule zote 47 za umoja.

Na kuzifungua tena tarehe 18 Desemba baada ya kusema kuwa imeimarisha mifumo ya kiusalama ndani na nje ya maeneo ya shule.

Hata hivyo, shule katika jimbo la niger bado zimefungwa huku serikali ya jimbo hilo ikisisitiza kuwa zitafunguliwa tu pale itakapokuwa na uhakika wa usalama wa wanafunzi na mazingira ya shule kwa ujumla.

Taarifa yake samba tenzi.

Ni rasmi makala ya 35 ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika imeanza kutimua vumbi jana nchini Morocco kwa wenyeji Morocco kuanza vyema na kushinda mchezo wa ufunguzi ambapo walifanikiwa kuifunga comoro mabao mawili kwa 0 mbele ya mashabiki wao katika uwanja wa rabat Morocco inatajwa kuwa miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu kushinda taji hilo sasa muda mfupi uliopita nimezungumza na mwandishi wa bbc, omary mkambara ambaye yuko nchini Morocco kutuletea yote yatakayojiri huko, lakini kwanza nilitaka kufahamu shamra shamra na maandalizi ya michuano iko vipi.

Martha shamrashamra ni kubwa na zimefanana kwa sababu ukishuka kwa mfano ya poti tu ukifika ya poti rabaa na sasa kuona picha muonekano kwamba afcon kweli inafanyika Moroko.

Kwa hiyo kimsingi Moroko waliokuwa mwili andaa na kila kitu kwenye siku ya.