Blog.

Radio Maria Tanzania - 2025-10-14T19:00:00.457Z

Radio Maria Tanzania

--:--
--:--

Transcription

Tutende tukapeleka ujumbe wa amani kwa watu wote.

The.

The.

Ni waimbaji wa kwaya ya mtakatifu kizito makuburi, wimbo wa amani na salama wanatufikisha 04:00 kamili usiku ninakukaribisha sasa usikilize marudio ya kipindi cha prolife titizo hai.

Injili ya uhai utamaduni wa kifo msikilizaji mpendwa radio maria Tanzania sauti ya Kikristo nyumbani mwako lina nakukaribisha katika kipindi cha prolife utetezi wa uhai kinachokujia kila siku ya Jumanne sana ni mchana na marudio yake 04:00 usiku studio namba 2 wapo wana pro life Tanzania wakiongozwa naye Anthony epa.

Grace shayo witness joakim pamoja na janet ya karo wanaendelea na mada kuu mwaliko wa kuwa mtetezi wa uhai ni lakini bado wanaendelea kukichambua kipengele kidogo cha utetezi wa uhai ni wito 1 kwa 1 niwapatie nafasi sasa ili waweze kutualika kwa kuomba kibali kwa Mungu.

Karibuni.

Kwa jina la baba na la mwana na la Roho Mtakatifu amina m Mungu Baba Mwenyezi uliathiri na mwanzo wa uhai wa kila binadamu.

Tunakushukuru kwa zawadi ya uhai unao tujalia pasipo mastahili yetu.

Tunakushukuru pia kwa ulinzi na baraka katika maisha yetu ndoa zetu na familia zetu umetuumba kwa sura na mfano wako umetuumba mwanaume na mwanamke na kwa njia ya sakramenti takatifu ya ndoa au anatushirikisha kazi yako ya uumbaji.

Watoto wanao tujalia kupitia upendo wa kindoa wanakuwa sio tu zawadi kwetu bali pia furaha na faraja katika mahusiano yetu ya kifamilia.

Ametukabidhi jukumu la kutangaza Injili ya uhai ambayo ni chemchemi ya matumaini yaliyovunjika na furaha ya kweli kwa kila kizazi Injili ya kweli kwa upendo wa Mungu na kwa wanadamu tunakuomba katika jukumu hilo la kutangaza Injili ya uhai na kwa maombezi ya mama Bikira Maria mtetezi wa uhai aliyetukuka utujalie neema na baraka ili tuweze kukabiliana na nguvu za wapinga uhai ndoa na familia hapa nchini kwetu na duniani kote kwa ujasiri na uthabiti mkubwa.

Hadi tufikie ushindi tunaomba hayo kwa njia ya Kristo bwana wetu amina kwa jina la baba na la mwana na la Roho Mtakatifu amina.

Ninawashukuru sana wana prof kwa sala ya ufunguzi msikilizaji mpendwa radio maria Tanzania sauti ya kikristu nyumbani mwako karibu uandike maoni yako kadiri ambavyo wana prof watakuwa akitufundisha kuhusiana na mada ndogo utetezi wa uhai ni wito kupitia namba 0734069967 andika ujumbe mfupi hapo 1 kwa 1 nami nitausoma kupitia redio maria Tanzania pamoja na mshirika redio sauti ya faraja kutoka bunena Kagera.

Mimi ni Elizabeth masanja kwa niaba ya wanapora of Tanzania.

Uhai zawadi ya Mungu mayai ya Mungu so upokee kwa ukarimu.

Upendo na shukrani.

Ni watu wa uhai na kwa ajili ya uhai.

Hongereni kwa utume, asante na kwako pia karibuni sasa mweze kurejelea kipindi kilichopita na kisha basi tuendelee kwa siku hii ya leo ninakukaribisha bwana antony epa asante sana dada Elizabeth masanja kwa ukaribisho mzuri na kutupa morali ya kutamka salamu yetu halikadhalika wale ambao walikuwa wamechoka choka na kukata tamaa bila shaka kupitia kipindi hiki watakuwa wapya tena.

Basi tunaendelea na.

Naye mada yetu ambayo kama tulivyosikia imetambulishwa mwaliko wa kuwa mtetezi wa uhai.

Na tupo katika kipengele kidogo cha utetezi wa uhai ni wito.

Na kipindi kilichopita tuliweza kuzungumza mambo kadhaa kwa nini utetezi wa uhai ni wito? Kwamba kuwa mwana uhai ni kuitikia wito wa kumtumikia Mwenyezi Mungu ambaye ndiye ametuumba sisi sote.

Ni Mungu anayetuita kutokana na upendo wake usiokuwa na mipaka kwa mwanadamu.

Kwa hiyo katika utume huu wa y.

Tunapohudumu nia na tunapokuwa wana uhai.

Maana yake tunatumikia.

Yale yote ambayo Mwenyezi Mungu ametupangia katika maisha yetu, kwa hivyo kila mmoja anaitwa kuwa mtetezi wa uhai, lakini kwa wale tu wanaokubali wito huo ndio wanakuwa wana uhai na ndio maana tunasema utetezi wa uhai ni wito.

Na kwa kila ambaye anatumikia kuwa mtetezi wa uhai basi amekubali na anakabidhiwa Injili ya uhai.

Ambayo msingi wake ni Yesu Kristo mwenyewe.

Na kila mmoja anaalikwa kuihubili na kuidhihirisha kwa vitendo akipewa nguvu za vipaji vya roho.

Na katika hali hiyo, mtetezi wa uhai anapofanya utume wake kikamilifu basi tunapata matunda katika maisha yetu.

Matunda hayo la kwanza tunapata furaha.

Tunapata upendo tunapata amani tunapata uvumilivu tunapata utu wema tunapata fadhili tunapata uaminifu tunapata upole tunapata na kiasi.

Hayo yote ni baadhi tu ya matunda ambayo mwana uhai anapoamua kuutumikia uhai kikamilifu basi anaongozwa na roho ya Mungu ambayo ndani yake inatengeneza hayo yote ambayo katika ulimwengu wa leo yanakuwa kuyapata ni changamoto upendo unakosekana furaha zinakosekana amani zinakosekana uvumilivu hatuna utu wema hakuna hayo yote ni kwa sababu wale ambao wanayatenda kinyume chake.

Sio wana uhai.

Na hata tukisoma katika kitabu kitakatifu cha wagalatia ile sura ya 5 aya ya 22 hadi 23rd inatueleza pale kwa kirefu matunda haya ambayo tunayapata kutokana na kuwa mwana uhai.

Kwa hiyo wito huu unaendelea.

Sio tu kwa mmoja mmoja lakini unakwenda hadi kwenye familia kwa hiyo mada mgesi naomba utuendelezee wito huu wetu katika nafasi ya kifamilia.

Asante sana.

Familia ina wajibu mahususi ambao unatokana na wito wake wa msingi kama jumuiya ya uhai na mapendo iliyojengwa katika msingi wa ndoa takatifu.

Katika familia kila mwanafamilia anampokea na kumjali kila mmoja kwa sababu hasa ya utu wake.

Familia ina wajibu mahususi katika maisha yote ya wanafamilia tangu kuzaliwa hadi kifo.

Huo ni wito wa utetezi wa uhai katika nafasi ya kifamilia dada witness naomba tu tushirikishe hapo wito huu wa utetezi wa uhai katika familia.

Familia ni kweli hifadhi awahi ni mahali ambapo huwahi kama zawadi itokayo kwa Mungu hupata karibu ya kweli na kukingwa dhidi ya mashambulizi mengi inayokabiliana nayo na hivi kuwezesha kukua katika misingi halisi ya kiutu.

Ndio kusema familia ni muhimu sana kiasi kwamba.

Nafasi yake katika kuijenga upya utamaduni wa uhai haiwezi kuchukuliwa na kitu kingine chochote.

Mmm wito huu wa utetezi wa uhai tukianzia kule kwenye familia.