Testimony FM - 2025-10-17T10:00:00.631Z
Testimony FM
Tabora
Transcription
Bw idhaa ya Kiswahili.
Inawakaribisha katika matangazo ya mchana.
Imetimia 07:00 kamili huko Afrika Mashariki 6 kamili Afrika ya kati sawa na hapa Ujerumani hujambo msikilizaji wa dw na karibu kwenye matangazo yetu ya mchana kwa niaba ya wenzangu wote watakaosikika jina langu ni bakari ubena.
Bw.
Habari za ulimwengu.
Msomaji mchana wa leo ni sylvia mwehozi kwanza muhtasari wake.
Rais trump kukutana leo na rais zelensky mjini Washington.
Urusi yashambulia gridi za umeme za Ukraine kwa droni na makombora.
Na ulinzi mkali waimarishwa Nairobi wakati maelfu wakijitokeza katika maombi ya kitaifa ya Raila Odinga.
Habari kamili Washington rais wa Ukraine, volodymyr zelensky anatarajiwa kukutana na rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya white house leo ijumaa.
Zelenski anatumai kupata idhini kutoka kwa Marekani kwa ajili ya uuzaji wa makombora ya masafa marefu ya Marekani ya tom work ambayo yanaiwezesha kuiruhusu Ukraine kuyatumia katika kuzima uvamizi wa urusi.
Zelenski amesema pia kwamba kasi iliyotumika baada ya makubaliano ya trump ya kusitisha mapigano kati ya kundi la wanamgambo wa kipalestina hamas.
Na Israel katika vita vya gaza inaweza kutoa msukumo mpya kwa mazungumzo ya kumaliza vita vya urusi nchini Ukraine siku 1 kabla ya mkutano wa leo, trump alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais wa urusi Vladimir putin na kusema kwamba anataka kukutana naye mjini budapest, hungary ndani ya wiki 2 zijazo.
Tff.
Urusi imeshambulia miundo mbinu ya nishati ya Ukraine kwa mamia ya droni na dazeni ya makombora katika mashambulizi yake ya hivi karibuni zaidi dhidi ya gridi za umeme za kiev mashambulizi hayo yamesababisha mikoa 8 ya Ukraine kukosa umeme huku kampuni kubwa ya binafsi ya nishati nchini humo detect ikiripoti kukatika umeme katika mji mkuu wa kiev na kusitisha uchimbaji gesi asilia katika mkoa wa kati wa poltava kutokana na mashambulizi, rais wa Ukraine volodymyr zelensky ambaye yuko ziarani Washington.
Marekani amesema urusi imerusha zaidi ya droni 300 na makombora 37 usiku kucha ameishutumu urusi kwa kutumia mabomu ya kutawanyika na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara yenye lengo 1 la kuwalenga wafanyakazi wa dharura na wahandisi wanarekebisha gridi za umeme.
Nairobi.
Maelfu ya waombolezaji wamehudhuria maombi ya kitaifa ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga leo huku ulinzi mkali ukiimarishwa baada ya hapo jana maafisa kufyatua risasi kutawanya umati wa watu waliojitokeza katika uwanja wa michezo wa kasarani kuaga mwili wake.
Odinga mwanasiasa mkongwe katika siasa za Kenya ambaye wakati mmoja alikuwa mfungwa wa kisiasa na kugombea urais mara 5 bila mafanikio alifariki dunia siku ya Jumatano akiwa na umri wa miaka 80 nchini india ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Odinga aliongoza kundi kubwa la wafuasi katika taifa hilo la Afrika Mashariki na umati mkubwa wa watu uliingia barabarani kuanzia mapema siku ya Alhamisi na kuvamia uwanja mkuu wa ndege wakati ndege iliyokuwa imebeba mwili wake ilipowasili.
Nataka kuupokea president wangu ambaye ni raila amolo odinga ametutoa mbali kama si raila hatungekuwa hapa kama si raila hatungekuwa na freedom of speech.
Vikosi vya usalama zilifyatua risasi hewani na polisi wakatumia gesi ya kutoa machozi kutawanya umati huo na hadi sasa polisi wanasema watu watatu wameuawa unaendelea kuisikiliza taarifa ya habari za ulimwengu kutoka dw antananarivo.
Kiongozi wa mapinduzi wa madagascar, kanali mikaeli ranjan irin ameapishwa leo kuwa rais wa nchi hiyo baada ya jeshi kuchukua mamlaka katika taifa hilo la kisiwa mapema wiki hii kufuatia maandamano walioongozwa na vijana ambayo yalimlazimu.
Rais andry rajoelina kukimbia nchi rajoelina ambaye wabunge walimtimua baada ya kutorokea nje ya nchi mwishoni mwa juma amelaani unyakuzi huo na kukataa kuachia madaraka licha ya uasi mkubwa katika vikosi vya usalama, Umoja wa Afrika na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Antonio guterres wamelaani mapinduzi hayo yaliyotokea baada ya wiki kadhaa za maandamano ya ujenzi.
Ranjan irin alisema hapo awali kwamba jeshi lilichukua mamlaka na kuvunja ta.
Sisi zote isipokuwa bunge la kitaifa.
Na hatimaye ni jerusalem Uturuki imetuma timu ya wataalam wa kushughulikia majanga kusaidia kutafuta miili iliyo chini ya vifusi huko gaza wakati rais Donald Trump wa Marekani akitoa onyo kwa hamas juu ya mfululizo wa mauaji ya hivi karibuni katika eneo hilo, trump ameyataja mauaji mauaji hayo kama ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano aliyaongoza ambapo kundi la wanamgambo la hamas iliwarudisha mateka 20 wa mwisho walionusurika kwa Israel.
Hamas imedai kuwa imerejesha 1,000,000.
Mateka lakini miili 19 bado haijulikani iliko na inaaminika kufunikwa chini ya magofu pamoja na idadi kubwa ya Wapalestina.
Hamas imesema kuwa inaheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel na wanataka kurejesha miili yote ya mateka iliyosalia gaza wataalam wa Uturuki watasaidia kuitafuta miili ya mateka huku familia zikasitishwa na hamas kwa kushindwa kurejesha miili ya jamaa zao.
Mwisho wa habari za ulimwengu kutoka dw.
Bw.
Dunia yetu.
Leo mchana.
Shukran sana sylvia mwehozi kwa taarifa ya habari za ulimwengu msikilizaji mchana huu tumekuandalia mengi katika uchambuzi wa ripoti zetu ikiwa ni pamoja na kiongozi wa kijeshi aliyefanya mapinduzi huko madagascar aapishwa rasmi kuwa rais na huko Nairobi.
Waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga aagwa kitaifa na urusi yafanya mashambulizi makubwa nchini Ukraine kwa hayo bila shaka na mengine mengi tafadhali usibadili kituo.
Msikilizaji tunathamini maoni yako ambayo ni muhimu sana kukamilisha matangazo haya unachotakiwa kufanya ni kutuandikia ujumbe mfupi kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na hata youtube tafuta dw Kiswahili nami nitausoma ujumbe wako hewani kadri muda utakavyoniruhusu.
Kiongozi wa mapinduzi wa madagascar, kanali Michael ranjan irin leo hii ameapishwa kuwa rais ikiwa ni ibada ya jeshi kuchukua madaraka kufuatia maandamano yaliyoongozwa na vijana ambayo yalimlazimisha rais aliyekuwepo madarakani andry rajoelina kukimbia kwenda uhamishoni sudi mnette na mengi zaidi kuhusu mkondo huu mpya wa siasa za madagascar katika hafla iliyofanyika katika mahakama ya juu ya katiba mjini antananarivo kanali mikael karanja ni lini amekula kiapo chake akisema atatimiza kikamilifu.
Kwa uadilifu na kwa haki majukumu makubwa nafasi yake mpya kama rais wa jamuhuri ya madagascar, mia niño.
Fahamu pia stand firm na tutui nitatimiza kikamilifu kwa ukamilifu na kwa haki majukumu makubwa ya nafasi yangu kama rais wa Jamhuri ya madagascar naapa kwamba nitatekeleza mamlaka niliyopewa na ninatoa nguvu zangu zote kulinda na kuimarisha Umoja wa kitaifa na haki za binadamu.
Kiasi chaka na.
Awali mapema kiongozi huyo alisema jeshi limechukua madaraka na kuvunja taasisi zote isipokuwa baraza la chini la bunge yaani bunge la kitaifa.
Alisema pia hakuwa kamati inayoongozwa na jeshi itatawala katika kipindi cha miaka miwili sambamba na serikali ya mpito kabla ya kuandaa uchaguzi mpya ranjan irini alikuwa kamanda wa kikosi maalum cha jeshi cha kapsaret ambacho kilihusika katika mapinduzi ya mwaka 2009 yaliyoleta madarakani ya rajoelina, lakini alijitenga naye wiki iliyopita.
Akiwahimiza wanajeshi wasiwapige waandamanaji wakati vijana wengi wakishangilia kuanguka kwa utawala wa argelina ambao uliingia madarakani kupitia mapinduzi kama haya.
Baadhi yao tayari wameonesha wasiwasi kuhusu kasi ya jeshi katika kufanikisha kuichukua nafasi ya uongozi.
Rajoelina ambaye wabunge walimuondoa madarakani baada ya kukimbilia nje ya nchi mwishoni mwa wiki hii amelaani mapinduzi.