Blog.

Magic FM Tanzania - 2025-10-17T04:00:00.460Z

Magic FM Tanzania

--:--
--:--

Transcription

Ambaye haja itumikia timu hiyo mchezo wowote tangu asajiliwe kutoka polisi Kenya kutokana na majeraha kumbe hajacheza sasa bila shaka ambao wawili simwoni we bwana huyu ni simuoni kumbe mmesajili mtu ana majeraha kutoka Kenya.

Muta ana majeraha kichwani asifanye hivyo bwana itakuwa kosa kwa nini limechukua mtu ana majeraha mnamuingiza kwenye.

Yeah.

3 nukta 3 maji kifahari men Dodoma.

Naam ni 01:00 kamili asubuhi.

Kata tayari kwa taarifa ya habari.

Hii ni taarifa ya habari kutoka maji kfm msomaji wako ni mimi nelson munema kwanza ni mukhtasari wake.

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa daktari philip isdor mpango azindua jengo na ifadhi ya urithi wa kiikolojia la Ngorongoro lengai.

Umoja wa ulaya kuimarisha ulinzi wa anga lake.

Na katika biashara taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania yatoa mafunzo kwa maafisa ugani habari kamili.

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, doctor philip isdori mpango amesema swala la utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi linapaswa kupewa kipaumbele katika uendelezaji na ukuzaji wa utalii ili kuepukana na kuvurugika kwa ekolojia na hatari dhidi ya ustawi wa shughuli za utalii.

Makamu wa rais amesema hayo wakati akizindua jengo la makumbusho ya eneo la hifadhi ya urithi wa kiikolojia la Ngorongoro lengai lililopo karatu mkoani Arusha.

Aidha makamu wa rais dokta mpango ametoa rai kwa wizara ya maliasili na utalii kupitia bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuhakikisha miundo mbinu ya makumbusho hayo inatunzwa na kutumika kama ilivyokusudiwa.

Wizara kwa kushirikiana na taasisi zake ikiwemo mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro ihakikishe inatoa mafunzo stahiki kwa watumishi watakaohudumu katika eneo hili ili kuwawezesha watumishi hao kutumia mifumo iliyopo na kutoa huduma kwa ufasaha na ufanisi.

Kwa upande wake waziri wa maliasili na utalii, balozi doctor pindi chana.

Amesema mageuzi makubwa yaliyofanyika katika wizara hiyo yamepelekea kuimarika kwa sekta ya utalii wa kuongeza watalii wa kimataifa kutoka 1,000,000 nukta 8 mwaka 2023 hadi kufikia watalii 2,000,000 nukta 1 kwa mwaka 2024.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa kassim majaliwa amesema kuwa serikali imedhamiria kuendelea kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema lengo la serikali ni kuendelea kuimarisha usalama wa chakula kupunguza utapiamlo na kujenga Tanzania yenye wananchi wenye afya bora, nguvu kazi, imara na uchumi unaojitegemea.

Amesema hayo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani tanga kwenye uwanja wa shule ya sekondari usagara.

Amesema kuwa serikali katika kuhakikisha imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo, iliongeza bajeti ya sekta hiyo kutoka shilingi bilioni 246 kwa mwaka 2020 21 hadi kufikia shilingi trilioni 1 nukta 3 kwa mwaka 2024 25.

Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya kilimo, gerald mwiri amesema kuwa kazi kubwa imefanywa na serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na rais daktari samia suluhu hassan katika uwekezaji kwenye sekta ya kilimo iliyowezesha kuifanya nchi kuwa na usalama wa chakula cha kutosha.

Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania jwtz limewahakikishia Watanzania kuwa hali ya usalama na utulivu nchini inaendelea kuwa shwari katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.

Katika taarifa iliyotolewa na kaimu mkurugenzi wa habari na uhusiano wa jeshi la wananchi wa Tanzania jwtz, kanali Bernard mlunga imeeleza kuwa jeshi litaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa usalama wa taifa na ninafurahishwa na jinsi hali ilivyo kwa sasa ambapo vyama vya siasa vinaendesha kampeni kwa kuzingatia sheria misingi ya heshima, uvumilivu na utulivu.

Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania linaviomba vyama vya siasa kuendeleza hali ya amani na utulivu wakati wote wa kampeni kupiga kura na baada ya kupiga kura.

Katika hatua nyingine, jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania linaipongeza jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama kwa jinsi vinavyoendelea kusimamia hali ya usalama katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Aidha jeshi hilo limetoa onyo kwa wanaotumia mitandao ya kijamii kupotosha umma na baadhi ya watu wanaharakati kutoka ndani na nje ya nchi wakilenga kulihusu.

Kisha jeshi na maswala ya kisiasa kwa lengo la kuvuruga amani ya taifa pamoja na hali ya amani na utulivu iliyopo bado kumeendelea kujitokeza baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati kutoka ndani na nje ya nchi kutumia mitandao ya kijamii kupotosha umma kwa kuweka maudhui yenye kuleta uchochezi kwa kulihusisha jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na siasa ili kutimiza azma yao ya uvunjifu wa amani.

Serikali imeeleza dhamira yake ya kutengeneza sheria rafiki za uwekezaji zitakazowezesha kufikia uchumi wa kati wa juu kama ilivyobainishwa kwenye dira 2050.

Hayo yamebainishwa jana wakati wa kikao kazi kati ya ofisi ya msajili wa hazina ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, ofisi ya wakili mkuu wa serikali na ofisi ya mwandishi mkuu wa sheria kilichofanyika kibaha mkoani Pwani.

Akizungumza katika kikao hicho.

Msajili wa hazina Nehemia mchechu amesema maagizo waliyopewa na rais daktari samia suluhu hassan ni uboreshwaji wa sheria ili ziendane na maono yaliyomo kwenye dira 2050.

Aidha, mchechu amesema serikali inataka kuona tija katika uwekezaji wake wa shilingi trilioni 92 nukta 3 uliofanywa katika taasisi za umma na kampuni ambazo ina umiliki wa hisa chache.

Naye naibu mwanasheria mkuu wa serikali, samuel maneno amesema kuwa uimara wa taasisi za umma na sekta binafsi unategemea ubora wa sheria zinazosimamia uwekezaji.

Unaendelea kusikiliza taarifa ya habari kutoka maji kifo m zifuatazo sasa ni habari za kimataifa.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa ulaya kaja class.

Amesema umoja huo hauna njia nyingine isipokuwa kuanzisha mfumo imara wa ulinzi wa anga ili kukabiliana na uchochezi wa droni za urusi.

Mpango huo unatarajiwa kuanza kufanyika kazi kikamilifu ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027.

Mpango huo ambao ni msukumo wa hivi punde katika harakati za kuimarisha ulinzi wa ulaya unatarajia kuidhinishwa katika mkutano wa kilele wiki ijayo.

Viongozi wa Umoja wa ulaya umezindua siku ya Alhamisi mpango huo kabambe wa kujiandaa na kile kinachofikiriwa kwamba kufikia mwaka 2030 kuna uwezekano wa kutokea mgogoro kati ya Urusi na nchi za Umoja wa ulaya.

Was it? Mkuu wa Israel, Benjamin netanyahu.

Amesema atahakikisha hamas inarejesha miili ya mateka waliosalia huku gaza akisisitiza kuwa mapambano bado hayajaisha.

Chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano iliyosainiwa na rais wa Marekani Donald Trump hamas.

Ilikabidhi Israel jana jumla ya miili 30 hivyo kufikia idadi ya jumla ya miili 120 ya mateka.

Miili ya mateka 19 bado haijulikani ilipo huku hamas ikisema inahitaji vifaa maalum ya kufikia magofu huko gaza ili kuipata miili hiyo ya mateka iliyosalia.

Kundi la kutetea mateka wa Israel limeitaka serikali ya nchi hiyo kuchelewesha hatua zitakazofuata na mpango wa amani iwapo hamas itashinda kurejesha miili hiyo.

Na sasa ni katika habari za biashara.

Kutokana na uzalishaji mdogo wa zao la mpunga visiwani Zanzibar.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, adam Kigoma ma.