RadioOne - 2025-12-19T04:00:00.471Z
RadioOne
Dar es Salaam
Transcription
Visa, Sunny Samoya Committee.
Tunakuletea taarifa ya habari msomaji ni amani lililo kwanza ni muhtasari wake.
Siku 1 baada ya serikali kuainisha mipango mikakati ya kutatua kero kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, baadhi ya wananchi mbali na kupongeza mipango hiyo wameiomba serikali hatua za utatuzi wa shida ya maji ufanyike haraka.
Polisi mkoani Mwanza inawashikilia watu 21 wakiwemo wanaoshiriki na kufanya shughuli za matambiko maarufu kama kamchape kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, uporaji na ubakaji.
Ujerumani imetangaza kuwa itawapokea raia wa Afghanistan wapatao 535 uliokuwa wameahidiwa kupewa hifadhi nchini Ujerumani, lakini hadi sasa wakiwa wamekamatwa katika hali ya sintofahamu nchini Pakistan.
Takriban watu 12 wameuawa na wengine watatu kutekwa baada ya watu wenye silaha kuvamia eneo la uchimbaji madini katika jimbo la Plateau katika katikati mwa Nigeria.
Tunaanza na habari za kitaifa.
Dar es Salaam.
Siku 1 baada ya serikali kuainisha mipango mikakati ya kutatua kero kubwa la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, baadhi ya wananchi mbalimbali na mbali na kupongeza mipango hiyo wameiomba serikali kutatua shida hiyo ya maji ifanyike kwa haraka.
Wananchi hao wamesema hayo katika mitaa mbalimbali ya jiji la dar es Salaam walipozungumza na radio one juu ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama wakiwemo wananchi wa vingunguti manispaa ya Ilala ambao wamedai maji.
Ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira dawasa kwa muda mrefu hawayapati kwa sasa wanatumia maji ya visima.
Kwa upande wao, wakazi wa kigogo kati wameomba kufufuliwa na kuendelezwa kwa visima vya dawasa vilivyokuwa katika mtaa huo vikitoa huduma ya maji safi ambavyo kwa sasa vimefungwa na havitoi maji kwa ajili ya wananchi wa mitaa hiyo.
Akiongea na radio one katika mahojiano maalum, waziri wa maji Mheshimiwa jumaa aweso ametaja mbinu ya utatuzi wa kero ya maji ikiwemo uboreshaji wa gridi ya taifa ya maji.
Nasio.
Polisi mkoani Mwanza inawashikilia watu 21 wakiwemo wanaoshiriki na kufanya shughuli za matambiko maarufu kama kamchape kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, uporaji na ubakaji.
Jeshi hilo linaendelea kuwasaka wengine na kuagiza wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kujisalimisha mara 1 kwa jeshi hilo.
Hatua hiyo ya jeshi la polisi inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kushamiri kwa matukio hayo.
Iliyosababishwa na kundi la waganga hao wanaojihusisha na ramli chonganishi ambapo wamekuwa wakitekeleza vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani katika vijiji vya kisiwa cha ukara.
Awali, kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, bwana wilbroad mutafungwa akizungumza na wakazi wa kisiwa hicho cha ukara amemweleza namna matukio hayo yalivyokuwa yakifanyika na kuathiri baadhi ya maisha ya wakazi wa kisiwa hicho pamoja na sababu za kuwaletea watu hao.
Kwenye vijiji vyao aidha kamanda mtafungwa amewataka wakaazi wa ukara na maeneo mengine ya mkoa Mwanza kuheshimu sheria na kuacha tabia ya kushiriki vitendo vinavyoweza uto.
Chato.
Mkuu wa mkoa wa geita bwana martin shigela ameagiza huvunji kuvunjiwa mkataba na kutozwa fedha za fidia.
Mkandarasi anayejenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita 17 zinazogharimu shilingi zaidi ya bilioni 20 kwa manispaa.
Gita hiyo inatokana na mkandarasi huyo kutekeleza ujenzi wa barabara hizo na kushindwa kukamilisha kwa wakati na kusababisha wananchi kupata adha kubwa katika usafiri.
Akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara wilayani chato mkoani geita.
Mkuu huyo wa mkoa amesema mkandarasi huyo avunjiwe mkataba na atafutwa mkandarasi mwingine ili wananchi wapate barabara.
Meneja wa wakala wa barabara mkoa wa geita bwana vedastus maribe ameiomba serikali kuwakamata watu wanaoiba miundombinu ya madaraja na alama za barabarani usiku wa manane na kuharibu madaraja.
Morogoro.
Serikali inakusudia kutumia maabara ya maabara ya taifa ya mbegu inayokarabatiwa kwenye taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania kurahisisha upimaji wa sampuli za mbegu pamoja na kuhakikisha mbegu hizo zinapata hadhi ya kuuzwa kimataifa na ikipiga marufuku.
Uuzaji holela wa mbegu kutokana na umuhimu wake, mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania, bwana chimagu nyasebwa amesema hayo baada ya katibu mkuu wa wizara ya kilimo kutembelea makao makuu ya ofisi hizo na kukabidhi magari manane kwa ajili ya shughuli za taasisi hiyo pamoja na kutembelea maabara hiyo ya taifa ya mbegu ambayo ukarabati wake unagharimu shilingi bilioni 83 umekamilika kwa 69/100.
Mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania, daktari liliane chambo licha ya kubainisha mikakati waliyonayo amezungumzia mahitaji ya mbegu na uzalishaji uliopo na umuhimu wa nchi kuwa na mbegu bora kwa ajili ya sababu mbalimbali ikiwemo mali ghafi za viwanda, usalama wa chakula na kuongeza kipato.
Unaendelea kusikiliza taarifa ya habari kutoka redio one zipatazo ni habari za kimataifa marin.
Ujerumani imetangaza kuwa itawapokea raia wa Afghanistan wapatao 535 waliokuwa wameahidiwa kupewa hifadhi nchini Ujerumani, lakini hadi sasa wakiwa wamekwama katika hali ya sintofahamu nchini Pakistan.
Waziri wa mambo ya ndani ya Ujerumani amesema wanatarajia kukamilisha mchakato wa kulishughulikia swala hilo mnamo mwezi huu Disemba ili kuwaruhusu watu hao kuwasili nchini Ujerumani.
Mpango huo uliidhinishwa na utawala uliopita.
Kwa kansela fredrick miez uliositisha mara tu alipoingia madarakani.
Lagos.
Takriban watu 12 wameuawa na wengine watatu kutekwa baada ya watu wenye silaha kuvamia eneo la uchimbaji madini katika jimbo la Plateau katikati mwa Nigeria.
Shambulio hilo lilitokea Jumanne jioni katika kijiji cha atoto wilaya ya fan eneo la serikali ya mtaa wakati wachimbaji migodi walipokuwa wakifanya shughuli ambazo wenyeji walieleza kama uchimbaji madini halali, kiongozi wa jamii ya Solomoni dailog.
Ameiambia bbc kuwa washambuliaji walifika kwa wingi na kufyatua risasi kiholela na kusababisha hofu na majeraha wengi.
Alisema waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali zilizopo karibu huku wakaazi waliachwa na majonzi na wakiwa mbioni kuwasaka waliochukuliwa.
Nairobi.
Seneta wa siaya na kiongozi wa ODM oburu oginga ametawazwa rasmi kuwa kiongozi wa jamii ya waluo wa Kenya wakati wa hafla iliyoandaliwa kaunti ya migori nchini humo.
Akizungumza baada ya tukio hilo, oburu alieleza heshima hiyo kama fursa kubwa akibadilisha kwamba amekubali jukumu hilo kwa unyenyekevu na dhamira ya juu ya uwajibikaji.
Akiongeza kuwa jambo hilo ni heshima kubwa kwake.
Akiwa ametawazwa rasmi kuwa kiongozi wa jamii ya waluo katika dimlitch mhina kaunti ya migori.
Aidha akasema kuwa anakubali jukumu hilo kwa unyenyekevu na kwa dhamira ya dhati ya kuhudumia kwa uadilifu, mshikamano na dhamira thabiti.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wanajamii wa waluo pamoja na viongozi wa eneo hilo akisisitiza umuhimu wake wa kitamaduni na kisiasa.
Kampala.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda bobi wine amemtaka rais wale Museveni asitumie nguvu kupita kiasi dhidi ya wananchi kabla ya uchaguzi ujao.
Katika ujumbe wake wa Twitter, bobi wine alisema kuwa harakati zake hakuwahi kuhamasisha vurugu mahali zinahamasisha maandamano ya amani haki ambayo ilihakikishiwa na katiba ya Uganda.
Alisisitiza kuwa wito huo ni kwa wananchi wa kawaida sio wahuni wanaofanya vurugu.
Bobi wine pia alisema kuwa wito wa maandamano ni sharti kama serikali itahakikisha uchaguzi huru wa haki na wazi basi hakutokuwa na haja ya maandamano alilaumu serikali ya Museveni kwa kudhibiti kampeni kuzuia upatikanaji wa vituo vya redio na kuwakamata wafanyakazi wa kampeni za upinzani.
Kwa kukamilisha taarifa ya habari huu tena muhtasari wake.
Siku 1 baada ya serikali kuainisha mipango mikakati ya kutatua kero kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.