Testimony FM - 2025-10-15T15:00:00.463Z
Testimony FM
Tabora
Transcription
DW.
Hili inawakaribisha katika matangazo ya jioni.
Naam tayari imetimia 12:00 kamili Afrika Mashariki karibu msikilizaji usikilize matangazo yetu ya jioni mimi ni jo.
Habari za ulimwengu.
Msomaji wako ni mimi bakari ubena lakini kwanza habari kwa ufupi.
Mawaziri wa ulinzi wa nato wakutana mjini brussels kujadili namna ya kujilinda na uchokozi wa urusi.
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin netanyahu warejea mahakamani kusikiliza kesi za ufisadi zinazomkabili.
Na Wakenya wanaendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga aliyefariki dunia hii leo.
Habari kamili, brussels.
Mawaziri wa ulinzi wa nchi wanachama wa jumuiya ya kujihami ya nato wanakutana mjini brussels Ubelgiji kujadili namna ya kujilinda na kukabiliana na vitisho na uchokozi wa urusi Umoja wa ulaya unashinikiza kuwepo na mfumo mpya wa kujilinda dhidi ya droni ambao utatakiwa kuanza kufanya kazi kikamilifu ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027.
Mwezi uliopita ndege za kivita za nato ziliungua droni za urusi zilizokuwa zimeingia kinyume cha sheria katika anga ya Poland.
Hii ni 1 kati ya mipango ya Umoja wa ulaya ambayo itazinduliwa rasmi kesho Alhamisi na inayolenga kuuandaa umoja huo na kile kinachotajwa kuwa kufikia mwaka 2030.
Kuna uwezekano wa kutokea kwa shambulio la urusi dhidi ya nchi za ulaya.
Tel aviv.
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin netanyahu amerejea tena hii leo katika mahakama ya tel aviv kusikiliza kesi ya ufisadi inayomkabili na iliyoanzishwa mei mwaka 2020.
Netanyahu alionekana mwenye tabasamu wakati yeye na msafara wake wa mawaziri kadhaa kutoka chama chake cha kihafidhina cha likud walipokuwa wakizomewa na waandamanaji wakati wakielekea mahakamani.
Katika 1 ya kesi netanyahu na mkewe sarah wanatuhumiwa kupokea bidhaa za kifahari zenye thamani ya zaidi ya dola laki 2 60,000 zikiwemo shampein sigara na vito kutoka kwa mabilionea kadhaa waliokuwa wakitaka kupewa upendeleo wa kisiasa.
Kesi hii inayomkabili netanyahu inajiri siku chache baada ya rais wa Marekani Donald Trump kupendekeza kwamba waziri mkuu huyo wa Israel anapaswa kusamehewa katika kesi zake.
3 tofauti za ufisadi.
Nairobi.
Taifa la Kenya linaendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa waziri mkuu raila amolo odinga aliyefariki dunia leo huko kerala nchini india.
Akiwa na umri wa miaka 80, polisi wa india wamesema odinga wamefariki kutokana na mshtuko wa moyo.
Mamia ya watu wamekusanyika kutoa heshima zao katika makaazi ya odinga jijini Nairobi, huku rais William Ruto akitangaza siku 7 za maombolezo na kuandaa mazishi ya kitaifa akimtaja odinga kama mwanasiasa hodari wa nchi ya Kenya.
I have declared a seventh ninatangaza kipindi cha siku 7 za maombolezo ya kitaifa ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti katika Jamhuri ya Kenya na katika balozi zetu zote nje ya nchi ni sherehe heshima kwake nimeahirisha shughuli zangu zote za umma kwa siku zijazo na ninawaomba pia viongozi na watumishi wengine wote wa umma kufanya vivyo hivyo n leaders.
Viongozi mbalimbali wa dunia kuanzia Afrika, Asia na kwingineko wametuma salamu zao za rambirambi kufuatia kifo cha kiongozi huyo ambaye ameiacha alama isiyofutika katika siasa za Kenya.
Ni taarifa ya habari za ulimwengu kutoka idhaa ya Kiswahili ya dw mjini bonn.
Roma.
Shirika la mpango wa chakula duniani wfp limetahadharisha hivi leo kuwa takriban watu 14,000,000 katika mataifa ya Afghanistan Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, haiti, Somalia, Sudan na Sudan Kusini wako hatarini kukumbwa na njaa kutokana na kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa ya kibinadamu.
Mkurugenzi mtendaji wa wfp cindy mccain amesema shirika hilo linatarajia mwaka huu wa 2025 kupokea chini ya 40/100 ya ufadhili ambazo ni sawa na dola bilioni 6 nukta.
4 kiwango ambacho ni kidogo mno na hakijawahi kushuhudiwa ukilinganisha na bajeti ya mwaka jana iliyofikia dola bilioni 10 chini ya utawala wa rais Donald Trump.
Marekani ambayo ndio mfadhili mkuu wa wfp ilipunguza kwa kiasi kikubwa misaada yake ya kigeni hatua iliyochukuliwa pia na mataifa mengine na hivyo kuathiri misheni za maendeleo na zile za misaada ya kibinadamu.
Na hatimaye antananarivo kiongozi mpya wa kijeshi wa madagascar, kanali Michael r andria nirina ataapishwa.
Rasmi kuwa rais wa nchi hiyo katika siku zijazo hayo yameelezwa na vyanzo viwili vya kuaminika baada ya kufanyika mapinduzi ya kumuondoa madarakani.
Rais andry rajoelina aliyekimbia nchi baada ya wiki kadhaa za maandamano ya umma kufuatia uhaba wa maji na kukatika kwa umeme.
Marekani imewatolea wito wadau wote nchini madagascar kutafuta suluhisho la amani linaloheshimu katiba baada ya kikosi maalum cha jeshi cha kapstat kutwaa madaraka.
Mwisho wa habari za ulimwengu kutoka dida ww mjini bonn.
Bw.
Dunia yetu.
Leo jioni.
William Ruto wa Kenya atangaza siku 7 za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga mashambulizi yaripotiwa huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo katika mkoa wa kivu kusini na malori ya misaada yaanza kuingia katika ukanda wa gaza.
Taarifa ya habari za ulimwengu imesomwa kwako na bakari ubena na kukaribisha hivi sasa tuanze safu hii ya uchambuzi wa ripoti zetu na tuanzie 1 kwa 1 huko nchini Kenya, rais William Ruto wa Kenya ametangaza kipindi cha maombolezi ya kitaifa kwa muda wa siku 7 kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga.
Katika kipindi hicho bendera za taifa zitapeperushwa nusu mlingoti kote nchini.
Na katika balozi zote za Kenya nje ya nchi kama ishara ya heshima na kumbukumbu ya kiongozi huyo aliyekuwa nguzo muhimu katika historia ya siasa za Kenya na bara zima la Afrika, shisia wasilwa na kina cha maelezo hayo.
Katika hotuba iliyotangazwa 1 kwa 1 kutoka ikulu jijini Nairobi, rais William Ruto alitangaza kuwa aliyekuwa kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement ODM Raila Odinga atazikwa kwa heshima kamili ya kitaifa.
Rais aliongeza kuwa jina la raila amolo odinga litaandikwa milele katika simulizi ya Jamhuri ya Kenya, simulizi ya mapambano kujitolea ujasiri, utawala, sheria, matumaini na azma ya ubora.
Ruto alimwelezea odinga kama mzalendo alijitolea maisha yake yote kutafuta haki nchini Kenya.
Mtu ambaye mawazo na misingi yake ilivuka mipaka ya siasa za kawaida.
We have lost party of common carriage tumempoteza mmoja wa viongozi wakuu zaidi barani Afrika shujaa wa demokrasia mpigania yake asiyeogopa na mwanaharakati thabiti wa utawala bora and servant of the people who gave his all wakati huo huo, rais ruto ametangaza kwamba serikali ya india imekubali kusaidia katika kusafirisha mwili wa Raila Odinga kurejea Kenya kwa mazishi ya kitaifa.
Kamati ya maandalizi ya mazishi ya aliyekuwa waziri huyo mkuu.
Itakuwa ikiongozwa na naibu rais kithure kindiki pamoja na seneta wa siaya dakta oburu oginga kakake marehemu ruto alifafanua zaidi kwamba ujumbe maalum wa maafisa wa serikali na jamaa wa familia unaoongozwa na waziri mwandamizi mswali mudavadi umeondoka tayari mara 1 kuelekea india kuratibu mipango, usafirishaji wa mwili wa marehemu hawa ni baadhi ya wabunge wakielezea hisia zao kuhusu msiba huo alikuwa rafiki wangu kutoka zamani nikiwa mwanahabari tulikuwa tunakutana naye mara kwa mara na alikuwa anatupa motisha twenty seventeen nilipotaka kuingia katika siasa.
Yeye ndio alikuwa mwanasiasa wa kwanza kunikumbatia kwa familia.
Kwa mama aidha.
Na wana ODM wote.
Kutokana na kifo hicho cha baba wetu, raila amolo odinga.
Imepaswa.
Kufanya cancellation.
Ya hafla ambayo ilikuwa imeanza jana wakati huo huo, viongozi wa kimataifa wameendelea kutuma salamu zao za rambirambi.
Waziri mkuu wa india, narendra modi alikokuwa akitibiwa raila amesema amehuzunishwa sana na kifo cha rafiki yake.
Mpendwa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, rais wa Tanzania samia suluhu alitangaza kwamba kifo cha odinga ni uzi.