Blog.

Habari Maalum FM - 2025-10-16T09:00:00.549Z

Habari Maalum FM

--:--
--:--

Transcription

Wanaendelea kutenda kwenye maisha yetu ni 06:00 kamili kama ambavyo tumesikia kiashiria muda mzuri wa neno la kweli twende tuka barikiwe na mtumishi wa Mungu sebastian peter kulisikia neno la Mungu na baada ya hapo tutakuwa tukiendelea kupokea ujumbe wako mfupi, kwa hiyo ambayo utakuwa wamekabidhi yesu maisha yako siku ya leo.

Mh.

Tunajifunza juu ya kutengeneza maisha tengeneza maisha yako na wakati mwingine tu wanalemewa na shida za dunia na changamoto mbalimbali eeh tunaona mizigo ni mizito ee lakini tukimkabidhi bwana tukitengeneza maisha yetu.

Tukimwambia Mungu shughulika na si shughulika na mahitaji yetu shughulika na mambo yote ambayo yanatuletea mmea tukimkabidhi yeye tukimkabidhi maisha yetu tukaamua kuokoka.

Kukabidhi yote kwake basi unaweza ukaona sio kwamba hutapita lakini katika kupita kwako itakuwa rahisi kwa sababu yuko Mungu ambaye atakuwa pamoja na wewe nimkaribishe sasa mtumishi wa Mungu karibu sana sebastian kwa ajili ya neno la Mungu na msikilizaji karibu tuweze kwenda pamoja kusikia kile ambacho Roho Mtakatifu ametuandalia kwa siku ya leo karibu sana.

Bwana Yesu asifiwe.

Basi ni siku nyingine njema ambayo Mungu ametusaidia.

Tumeweza kuifikia.

Ni kwa neema yake wala si kwa ujanja wala nguvu zetu.

Na ninaamini hivyo hivyo pia kwa ndugu msikilizaji kwamba Mungu amekupa uzima ni kwa neema zake.

Wala si kwa sababu ya juhudi au maarifa uliyo nayo? Kuweza kusema kwamba umeweza kufika siku ya leo.

Sasa tunaenda kujifunza neno la Mungu.

Na kabla ya kuendelea ningependa sasa nimshukuru Mungu halafu tutaendelea kujifunza kwa pamoja baba katika jina la Yesu Kristo, jina lipitalo majina yote asante kwa ajili ya siku njema ya leo ambao umetusaidia watoto wako kuifikia ni siku njema na ya baraka ebwana ambayo haijawahi kutokea mwokozi wetu uliyehai tunakurudishia sifa na heshima na shukrani kwa ajili ya ukuu wako kwenye maisha yetu katika jina la Yesu Kristo.

Ninakushukuru kwa ajili ya ndugu msikilizaji ambaye anafuatilia bwana mafundisho haya ninaomba neema yako ikazidi kuwa pamoja naye ukawafunike kwa nguvu zako na uweza wako umuepushe na kila distraction yoyote na roho yoyote aagiza kwa china la Yesu Kristo neema yako ikapate kumfunika ee bwana na hatimaye akajifunze kile ambacho amekiandaa kwa ajili yake.

Kwa siku hii ya leo.

Asante kwa sababu Roho Mtakatifu upo pamoja nasi kupitia jina la baba na la mwana na la Roho Mtakatifu.

Amen.

Basi ndugu msikilizaji kwa majina yangu naitwa mtumishi wa Mungu, sebastian peter.

Eeh tupo pamoja katika kipindi hiki na tutaenda kujifunza neno la Mungu ambalo linasema ama lenye kichwa cha somo kinachosema tengeneza maisha yako tengeneza maisha yako.

Kwani tunajifunza kwa habari ya kutengeneza maisha? Mtu anayeambiwa kwamba atengeneze kitu fulani atengeneze labda mlango watengeneze eeh chombo fulani maana yake kimeharibika au ku kuna changamoto hakifanyi kazi kama inavyopaswa au hakitimizi yale majukumu yake ya kila siku.

Kama ni simu itengenezwe maana yake ina shida au ina kasoro fulani.

Sasa ujumbe wetu unasema kwamba tutengeneze a utengeneze maisha yako kwa maana hiyo maisha yako yameharibika.

Kwa nini maisha yameharibika sasa tunaenda kuona tutasoma katika.

Vitabu viwili lakini nitaanza na kimojawapo ambacho ni Petro wa pili ile sura yake ya 3 kuanzia mstari wa 3 nitasoma mistari kadhaa hapo na baadaye tena nitasoma kitabu kingine ili tuweze kujifunza kwa pamoja.

Kama una Biblia yako eeh na unafuatilia somo hili unaweza ukafungua pamoja nami katika kitabu cha Petro wa pili sura yake ya 3 na kuanzia mstari wake wa 3.

Neno la Mungu linasema.

Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja.

A na dhihaka zao watu wenye kudhihaki wafuatao tamaa zao wenyewe.

Na kusema iko wapi ahadi ile ya kuja kwake.

Kwa maana tangu.

Hapo baba zetu walipolala vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo tangu mwanzo wa kuumbwa.

Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani na nchi pia imefanyizwa kutoka katika maji na ndani ya maji kwa neno la Mungu.

Kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji ikaangamia.

Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto kwa neno lilo hilo zikilindwa hata siku ya hukumu na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.

Lakini wapenzi msilisahau neno hili kwamba kwa bwana siku 1 ni kama miaka elfu.

Na miaka elfu ni kama siku 1.

Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake kama wengine wanavyokudhani kukawia bali huvumilia kwenu maana hapendi mtu yeyote apotee bali wote waifikilie toba.

Lakini siku ya bwana itakuja kama mwivi katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu na viumbe vya asili vitaunguzwa na kufumuliwa na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

Bas kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa.

Bwana Yesu asifiwe sana mtu wa Mungu.

Hapa tunajifunza neno la Mungu na kumbuka nimesema kichwa cha somo kinasema kwamba tengeneza maisha yako.

Neno la Mungu linatuambia ya kwamba kuna watu katika nyakati za mwisho.

Ee tunapofikia nyakati za mwisho za eeh dunia hii kutatokea watu ambao watakuwa na maneno ya dhihaka ambao watakuwa wakituambia sisi tunaomwamini Mungu kwamba yuko wapi sasa yule yesu wenu ambaye alisema kwamba anarudi mbona siku zinazidi kwenda mbona miaka inazidi kwenda mbona nyakati zinakuja vitu vipo? Vile vile majira yanakuja majira yanarudi yapo vile vile.

Wala yesu wenu ambaye aliyewaahidi kwamba atarudi bado hajarudi sasa neno la Mungu linatupa ufafanuzi ya kwamba mbona watu hawa wanajisahaulisha kwamba kuna dunia hii hii ambayo imeumbwa na Mungu kuna nyakati fulani ambazo wanadamu walipo amsahau Mungu wanadamu walipokaa mbali na uso wa Mungu.

Mungu akaamua kuiga rikisha dunia kwa maji, watu waliangamizwa wale ambao.

Walikuwa wamemkaidi Mungu wale ambao walikuwa wakienda kinyume na Mungu wale ambao walikuwa hawamchi Mungu.

Maana yake, tunapozungumza kwa habari ya kutengeneza ni kama hivi.

Kumcha Mungu kumrudia Mungu wetu aliye hai huyo ndiye baba yetu aliyetuumba huyu ndiye mfalme wetu tunayepaswa kumtumikia lakini maisha ya wanadamu yameharibiwa na kutokumcha Mungu yameharibiwa kwa kutegemea miungu kwa kutegemea wachawi kwa kutegemea waganga yameharibiwa kwa kutokutegemea Mungu ambaye amewaomba kwa mfano na kwa sura yao sawa na mwanzo.

1 26.

Sasa.

Mungu anasema ya kwamba utengeneze maisha yako kwa sababu ataweza kuangamiza.

Kama ilivyosema katika neno la Mungu ya kwamba dunia ya wakati ule au nyakati zile iliangamizwa kwa gharika ya maji.

Lakini dunia ya wakati huu au kizazi hiki kimeandaliwa ama kimewekewa akiba ya moto kwa wale wote ambao watakuwa hamjui hawamchi Mungu kwa wale wote ambao hawana muda na Mungu wao wanaendelea na bize sow wanaendelea na nasa zao.

Maana Biblia inasema ya kwamba mtu yeyote ambaye anaipenda dunia na mambo yake kumpenda baba hakumo ndani yake.

Sasa watu kama hao.

Ambao hawamtii Mungu ambao hawana muda na Mungu ambao Biblia inasema kwamba mpumbavu husema moyoni mwake ya kwamba hakuna Mungu.

Sasa watu kama hawa ambao wanasema hakuna Mungu wanasema kwamba yesu atarudi wanasema ya kwamba hakuna Mungu wala hatutafanya kitu chochote wala hatuta aangamizwa Biblia inasema ya kwamba watu kama hao nyakati zinakuja.