Radio Uhai - 2025-12-19T10:00:00.523Z
Radio Uhai
Tabora
Transcription
Msikilizaji muda mfupi kutoka sasa tutajiunga na idhaa ya Kiswahili ya dw kutoka bonn Ujerumani hii ni redio ya uhai 94 nukta 1 Tabora.
Bw idhaa ya Kiswahili.
Inawakaribisha katika matangazo ya mchana.
Hujambo popote pale ulipo imekwisha atumia 07:00 kamili Afrika Mashariki 6 Afrika ya kati lakini ni 05:00 asubuhi hapa mjini bonn hujambo na karibu kwenye matangazo yetu ya mchana.
Bw.
Habari za ulimwengu.
Kwanza lakini ni habari kwa ufupi msomaji ni babu Abdallah.
Umoja wa ulaya watoa mkopo usiokuwa na riba wa euro bilioni 90 kuisaidia Ukraine katika vita vyake dhidi ya urusi.
Wanamgambo wa rsf wamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1000 nchini sudan ndani ya siku 3.
Karibu watu nusu 1,000,000 wameyakimbia makazi yao jimbo la kivu kusini tangu mwanzoni mwa mwezi Disemba.
Habari Chameleon, Brussels.
Viongozi wa Umoja wa ulaya wamekubaliana kutoa mkopo usiokuwa na riba wa euro bilioni 90 kwa Ukraine ili kusaidia mahitaji yake ya kijeshi na kiuchumi katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Hata hivyo, viongozi hao bado hawajafikia muafaka na Ubelgiji kuhusu pendekezo la kutumia mali za urusi zilizozuiwa ndani ya umoja huo kama chanzo cha kukusanya fedha za mkopo huo.
Rais wa Ufaransa, Emmanuel macron amesema makubaliano hayo ni hatua muhimu mbele.
Akibainisha kuwa kukopa kupitia masoko ya mitaji ndio chanzo halisi na kinachowezekana zaidi kwa wakati huu ili kuiunga.
Uamuzi huo wa viongozi wa Umoja wa ulaya.
Ogopa.
Kisha uwezo na mamlaka yake tunasimama imara dhidi ya tishio kubwa zaidi kwa usalama barani ulaya.
Uchokozi wa urusi ambao kwa muda mrefu umevuka mipaka zaidi ya uvamizi dhidi ya Ukraine.
Baada ya takriban miaka minne ya vita, shirika la fedha la kimataifa linakadiria kuwa Ukraine itahitaji euro bilioni 137 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Brussels cancel of Germany.
Frederich, Man.
Arts na rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya, ursula for dean wameeleza matumaini kuwa Umoja wa ulaya utaweza kusaini makubaliano tata ya biashara huria na Muungano wa Amerika Kusini mwezi Januari.
Hii ni licha ya kukosekana kwa uungaji mkono wa kutosha katika mkutano wa kilele wa umoja huo, founder lyon alitarajiwa kusafiri kwenda Brazil kwa hafla ya kutia saini makubaliano kesho Jumamosi, lakini hilo.
Nilitegemea idhini ya idadi kubwa ya nchi wanachama.
Geneva.
Mashirika ya misaada katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo yamesema kuwa mapigano yanayoendelea yamesababisha maelfu ya watu kuyahama makaazi yao.
Valeria kakavu kutoka shirika la Msalaba Mwekundu mjini bukavu amesema kuwa mapigano yaliyotokea mwezi huu yamekuwa makali zaidi kuliko ilivyokuwa awali.
Shirika hilo limeongeza kuwa machafuko katika maeneo mbalimbali ya jimbo la kivu kusini yanaendelea kusababisha vifo na kuwalazimisha maelfu ya wakaazi kuyakimbia makazi yao kwa hofu ya usalama.
Tangu mwanzoni mwa Desemba zaidi ya watu 100 wenye majeraha ya risasi wametibiwa katika hospitali zinazosaidiwa na Msalaba Mwekundu jimbo la kivu kusini.
Khartoum.
Wanamgambo wa kikosi cha rsf ambao wamevuka wamekuwa vitani na jeshi la serikali kwa muda wa miaka miwili na nusu walisababisha vifo vya zaidi ya watu 1000 wakati wa mashambulizi ya siku 3 waliyoyafanya mwezi Aprili hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa mataifa iliyotolewa jana ofisi ya Umoja wa mataifa ya haki za binadamu imeeleza katika ripoti yake kwamba ilirekodi mauaji ya raia 1013.
Wakati wa mashambulizi ya rsf kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya zamzam kati ya 04/11 na 13.
Unaendelea kuisikiliza taarifa hii ya habari za ulimwengu inayokujia 1 kwa 1 kutoka idhaa ya Kiswahili ya dw bonn.
Washington.
Waziri wa usalama wa ndani wa Marekani christino m ameusimamisha mpango wa bahati nasibu wa uhamiaji maarufu green card lottery akisema mpango huo ulitumika na mtuhumiwa wa shambulio la risasi katika chuo kikuu cha brown noem ameandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba mshukiwa huyo manuel neves valente.
Aliingia Marekani kupitia mpango wa bahati nasibu ya visa ya uhamiaji mnamo mwaka wa 2017 na baadaye kupewa kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini humo.
Amesema ameusimamisha mpango huo ili kuhakikisha kuna umarekani zaidi watakaoathirika na huo ndio mwisho wa taarifa hii ya habari za ulimwengu iliyokujia 1 kwa 1 kutoka idhaa ya Kiswahili ya dw bonn.
DW.
Dunia yetu.
Leo mchana.
Nchini huu tutaanza na mkutano wa viongozi wa Umoja wa ulaya waliopitisha mpango wa kuisaidia Ukraine kifedha lakini wameshindwa kuafikiana kuhusu njia ama namna ya kutumia mali za urusi kuifadhili Ukraine.
Kisha tutawamulika Tanzania shirika la kutetea haki za binadamu la amnesty International linasema vikosi vya usalama vya nchi hiyo vilitumia nguvu kupita kiasi na hata kuwaua waandamanaji wakati vurumai ilipozuka wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
Na nchini Uganda rais Yoweri Museveni amekosolewa vikali kwa matamshi yake ya kuwatisha waandamanaji kuhusu uwezo wa polisi na wanajeshi kutumia risasi.
Tuandikie maoni yako kuhusu taarifa utakazo zisikiliza mfuatiliaji wetu, lakini kama nilivyo kuarifu tunaanzia hapa barani ulaya, viongozi wa Umoja wa ulaya mapema hii leo wamefikia makubaliano ya kuipatia Ukraine mkopo wa euro 90,000,000 ili kufidia mapungufu yaliyoko kwenye bajeti yake lakini wameshindwa kukubaliana kutumia mali za urusi zilizofungiwa ili kutoa ufadhili huo.
Jacob safari ana mengi zaidi katika ripoti ifuatayo.
Makubaliano hayo yaliyofikiwa usiku wa manane katika mkutano wa kilele uliofanyika huko brussels, Ubelgiji yanaipa Ukraine nguvu mpya ilizokuwa inazihitaji mno wakati wa rais wa Marekani Donald Trump anashinikiza kupatikana kwa makubaliano ya kusitisha kwa haraka vita hivyo vya Ukraine na urusi vilivyodumu kwa takriban miaka minne huku Ukraine ikiwa imeshushwa mabega kidogo na hatua ya Umoja wa ulaya kutofikia makubaliano ya kutumia mali za urusi kupatikana kwa ufadhili.
Kwa njia nyingine pia ni ahueni.
Hii ni kwa kuwa mwanzoni mwa mkutano huo wa kilele rais wa Ukraine volodymyr zelensky alikuwa amewaambia viongozi hao wa ulaya kuwa kunahitajika uamuzi kufikia mwisho wa mwaka na kwamba kuiweka nchi yake katika nafasi yenye nguvu kutoipatia fursa nzuri kwenye mazungumzo ya kusitisha vita.
Antonio costa ni rais wa baraza la ulaya.
We have agreed to row.
Over awe sanctions tumekubaliana kuweka vikwazo dhidi ya urusi lengo letu si kurefusha vita isitoshe maamuzi ya leo ni mchango muhimu katika kupatikana kwa amani ya haki na ya kudumu nchini Ukraine kwa sababu njia ya pekee ya kuileta urusi kwenye meza ya mazungumzo ni kwa kuimarisha Ukraine.
Is to strengthen Ukraine.
Zelensky katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii, wa x ameyasifu makubaliano hayo akisema ni muhimu kwa kuwa nchi yake imepokea hakikisho la ufadhili kwa miaka ijayo majadiliano kuhusu kuipa ji Ukraine mkopo kutokana na mali za urusi yalikuwa magumu na wazo la ufadhili huo kupatikana kwa ulaya kuomba mkopo awali lilionekana kama lisilowezekana kwani ni jambo linalohitaji makubaliano ya pamoja na hungary ambayo waziri wake mkuu victor orban ni mwandani wa rais Vladimir putin ilikuwa amelipinga.
Kila hungary pamoja na Slovakia na Jamhuri ya chek baadaye walikubali mpango huo wa mkopo usonge mbele mradi tu usioathiri kifedha kigingi kikuu kilikuwa kuipa Ubelgiji hakikisho la kuto.