Radio Kwizera - 2025-12-20T10:00:00.694Z
Radio Kwizera
Ngara
Transcription
Unaendelea kuisikiliza redio kwizera fm stereo msikilizaji wakati wowote kuanzia hivi sasa tutajiunga na radio dot vile.
Katika matangazo ya mchana.
Imetimia 07:00 kamili huko Afrika Mashariki sawa na 6 kamili huko Afrika ya kati hujambo na karibu katika matangazo ya dw kutoka hapa mjini bonn.
Bw.
Habari za ulimwengu.
Kwanza ni muhtasari wa habari hizo, msomaji wako ni mimi bakari ubena watu wanane wauawa odessa kufuatia mashambulizi ya urusi huko Ukraine pia ikishambulia kwa droni baraza la usalama la Umoja wa mataifa la akiongezea muda wa mwaka mmoja kikosi cha monusco huko drc na waziri mkuu wa Australia amesema jamii ya Wayahudi nchini humo iko imara na haiwezi kusambaratishwa.
Habari kamili, kiev.
Takriban watu wanane wameuawa na wengine 27 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la kombora la urusi usiku wa kuamkia leo katika mji wa bandari wa odessa nchini Ukraine basi la abiria lililengwa huku malori yakiwaka moto katika eneo la maegesho ya magari.
Taarifa hiyo ilitolewa na huduma ya ulinzi wa Ukraine haikuweza kuthibitishwa na vyanzo huru vya habari.
Pia jeshi la Ukraine limesema limeshambulia kwa droni na kuharibu kituo cha kuchimba mafuta cha lukole pamoja na meli ya kivita ya Urusi ya ocho tznic.
Katika Bahari ya caspian takriban kilomita 1800 kutoka Pwani ya Ukraine, hayo yakiarifiwa mjumbe wa urusi, kirill dmitrieva, amesema hivi leo kuwa anaelekea katika mji wa miami nchini Marekani ambako duru nyingine ya mazungumzo ya kujaribu kuutatua mzozo wa Ukraine imepangwa kufanyika.
New York.
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limepitisha kwa kauli 1 azimio la kuongeza muda wa kuhudumu kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo monusco azimio hilo lilipigiwa kura hapo jana na kikosi hicho kimeongezewa muda wa mwaka mmoja wa ziada hadi 12/20 mwaka 2026 huku Marekani ikitoa wito kwa vikosi vya Rwanda na waasi wa m 23 kuheshimu makubaliano ya amani ya kikanda kufuatia vurugu zinazoendelea kushuhudiwa mashariki mwa drc.
Mwakilishi wa Marekani katika mkutano huo, Jennifer luchita amesema mazungumzo ya kuiongezea muda monusco yalitiwa kiwingu na mwenendo wa Rwanda na waasi wa m 23.
Kwa kuhojiwa mchakato thabiti wa amani kikosi cha monusco chenye wanajeshi 11,500 ni 1 ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa mataifa vinavyoungwa mkono na Marekani.
Lakini utawala wa rais Donald Trump ulijaribu kupunguza mchango wake wa kifedha kwa Umoja wa mataifa hasa katika eneo la ulinzi wa amani duniani.
Sydney.
Waziri mkuu wa Australia, Anthony albanese amesema jamii ya Wayahudi nchini humo iko imara na haiwezi kusambaratishwa.
Alibainisha ameitoa kauli hiyo leo baada ya kuhudhuria ibada katika sinagogi mjini sydney kwa ajili ya maombolezo ya waathiriwa wa shambulio la risasi lililotokea wakati wa sherehe ya hanuka kwenye ufukwe wa bondy Jumapili iliyopita.
Tukio hilo lililosababisha vifo vya watu 15 ni baya zaidi nchini Australia kwa karibu miongo mitatu.
Na sasa linachunguzwa kama kitendo cha ugaidi dhidi ya Wayahudi mamlaka za Australia zimeimarisha ulinzi kote nchini humo na kuweka sheria kali zaidi ya umiliki wa bunduki ili kuzuia vitendo kama hivyo ni taarifa ya habari za ulimwengu kutoka idhaa ya Kiswahili ya dw o mjini bonn.
Geneva.
Rais wa zamani wa iraq, barham salih ameteuliwa kuwa mkuu mpya wa shirika la Umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR akichukua nafasi ya filipo grandi raia wa Italia aliyeshikilia nafasi hiyo kwa miaka 10.
Shirika hilo la wakimbizi lenye makao yake makuu mjini geneva nchini Uswisi huwasaidia mamilioni ya watu kote duniani ambao wamelazimika kuzikimbia nchi zao kutokana na vita na madhila mbalimbali.
Uteuzi wa salehe mwenye umri wa miaka 65 ulifanyika siku ya Alhamisi baada ya jina lake kupendekezwa na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Antonio guterres na kuthibitishwa rasmi na baraza kuu la Umoja wa mataifa mjini New York rais huyo wa zamani wa iraq anachukua uongozi wa shirika ambalo linakabiliwa na tatizo kubwa la ufa.
2 huku idadi ya wakimbizi ikiongezeka zaidi kutokana na vita na migogoro nchini Ukraine, Afghanistan, drc Sudan na nchi nyingine nyingi.
Na hatimaye, athens.
Mamia ya wahamiaji wamewasili katika kisiwa cha Ugiriki cha crete kwa kutumia mashua katika muda wa siku 2 zilizopita boti za doria za walinzi wa Pwani wa Ugiriki na zile za shirika la ulinzi wa mipaka barani ulaya frontex zimeokoa baharini wahamiaji zaidi ya 650.
Watu hao walipelekwa kwenye kambi mbalimbali za wakimbizi kisiwani humo.
Hali ya hewa tulivu iliyoshuhudiwa eneo hilo imepelekea wasafirishaji haramu kutuma boti zaidi kuelekea barani ulaya.
Huku idadi kubwa ya boti hizo zikitokea katika bandari ya libya ya tobruk mwaka huu pekee kisiwa cha crete kimepokea takriban wahamiaji 18,000 ikilinganishwa na 5000 mwaka jana.
Mwisho wa habari za ulimwengu kutoka bonn.
Bw.
Naam hujambo msikilizaji na karibu kwenye meza ya duara leo hii wataalamu wetu wanajadili siasa za nchini Uganda wakati ambapo nchi hiyo inaelekea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika 01/15 mwaka ujao wa 2026.
Asasi za kiraia, wadadisi wa maswala ya utawala na wanasiasa na watu mbalimbali wanakosoa uhusika wa 1 kwa 1 wa wanajeshi katika uchaguzi nchini Uganda.
Matukio ya wanajeshi wanaoshuhudiwa kushirikiana na polisi katika kuwadhibiti wagombea.
Na wafuasi wa upinzani wanapoendesha kampeni zao kwa ajili ya uchaguzi mkuu pamoja na kauli zinazotolewa na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu jeshini hayo yanazingatiwa kuwa jeshi linasimamia uchaguzi badala ya tume ya uchaguzi.
Je ni kwa nini tume ya uchaguzi haijajitokeza waziwazi na kudhihirisha kuwa ndiyo yenye mamlaka juu ya maswala ya uchaguzi wanasheria nao kwa upande wao wameihimiza tume ya uchaguzi kuzingatia katiba na kufahamu kuwa uchaguzi ni swala nyeti.
Na haki za binadamu na kwa upande wao baadhi ya wafuasi wa chama tawala cha nrm wanasisitiza kuwa ni muhimu polisi kupata usaidizi wa jeshi ili kuhakikisha utulivu unakuwepo katika kipindi cha uchaguzi na hatua kama hii sio kinyume cha katiba ya nchi.
Kwa ufupi msikilizaji kampeni za uchaguzi nchini Uganda zimepamba moto na wachambuzi watajadili hayo na mengineyo kuhusu uchaguzi huo.
Na sasa nachukua fursa hii kuwatambulisha wachambuzi wetu kwenye maoni meza ya duara leo hii kutoka jijini Kampala nchini Uganda tunaye leo mstaafu kapten Francis babu mchambuzi wa maswala ya kisiasa vile vile kutoka Shinyanga nchini Tanzania nimemkaribisha tumaini munale.
Yeye ni mkufunzi wa chuo cha ualimu mjini Shinyanga ni mchambuzi wa maswala.
Ya siasa za barani Afrika na vile vile za kimataifa watatu ni ally mutasa, mwandishi wa habari na mchambuzi wa maswala ya kisiasa.
Yeye yupo jijini Kampala vile vile nchini Uganda studio hapa ninaye mwenzangu idd cisanga ambaye tutakuwa pamoja katika kipindi hiki na mimi ni zainab aziz mwenyekiti wako kutoka hapa dw bon na 1 kwa 1 nianze labda.
Na wewe iddy cisanga unazungumzia vipi kuhusu mazingira ya siasa kwa jumla katika siasa za nchini Uganda kuelekea kwenye uchaguzi? Asante bi zainab labda swali hili lingeanza na walioko Uganda, lakini kwa vile umenichagua mimi nianze nitasema ni mazingira kwanza ni nilikuwepo siku chache zilizopita nilikuwa Uganda na nimeshuhudia baadhi ya matukio ya kampeni, lakini ninaweza kusema ni mazingira.
Tete ya ushindani mkubwa lakini pia swala lilitaja la washiriki wa vyombo vya usalama ni kubwa hasa kwa upande wa chama cha upinzani.
Chama cha National unity platform nimeshuhudia baadhi ya matukio yake ya kampeni mmojawapo alikuwa mgombea wake akiondoka kwenye makao makuu ya chama.