Shalom FM 97.3 - 2025-11-25T07:00:00.525Z
Shalom FM 97.3
Arusha
Transcription
90 7 .3 Shalom FM.
Hivi sasa ni 04:00 asubuhi.
Ikiwemo msikilizaji hujambo na karibu sana katika habari za biashara na uchumi kutoka hapa.
Shalom fm.
Jina langu ni William obando na tuanzie hapa mkoani Arusha.
Benki kuu ya Tanzania bi OT imeratibu mkutano wa kamati ya ufundi ya tehama katika maswala ya fedha kwa benki kuu za nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano huo wa siku 4 umefunguliwa jana 11/24 na meneja wa idara ya uchumi tawi la BOT Arusha bwana eris tides mrema kwa niaba ya mkurugenzi wa tawi hilo.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, mkurugenzi wa mifumo ya mawasiliano bi ot bwana bwana joel ngusa amesema lengo kuu la warsha hiyo ni kubadilishana uzoefu ulinganifu usimamizi wa tehama na kuandaa mapendekezo yanayoweza kutekelezeka ambayo yataimarisha usimamizi wa mifumo katika benki kuu wanachama.
Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe kutoka nchi wanachama za jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo.
Dar es Salaam.
Serikali imepanga kuongeza maeneo maalum ya uwekezaji kongani nchini hatua inayolenga kuchochea uzalishaji kuongeza tija na kuboresha mazingira ya kufanya biashara.
Akizungumza mkoani dar es Salaam alipotembelea tume ya ushindani, waziri wa viwanda na biashara, judithi kapinga amesema siri sekta ya viwanda imeendelea kukua na kuimarika hususani katika uzalishaji wa malighafi unaochangia maendeleo ya uchumi wa taifa.
Waziri akapinga amebainisha kuwa serikali inaendelea kupanua wigo wa viwanda ili kukuza ajira kuongeza mapato ya ndani na kupanua mauzo ya nje kupitia utekelezaji wa sera endelevu zinazolenga kukuza sekta hiyo.
Aidha amesema kuimarishwa kwa viwanda kutachochea ongezeko la uzalishaji wa malighafi hatua itakayoongeza mapato na kuendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa wawekezaji na wajasiriamali.
Mikakati ambayo tunayo serikali la kwanza kuendelea kuongeza kongani za viwanda kwa sababu tunaamini kupitia viwanda tutaongeza tu mapato ya nje lakini hivyo tutaongeza ajira.
Tutaongeza mapato ya ndani lakini vile vile kuendelea kutekeleza sera zetu ambazo ni himilivu, tunazo sera ambazo ni kula, lakini vile vile tumekuwa tukija na sera mbalimbali kulingana na mabadiliko ya mazingira ya biashara ambayo yanakuja mara kwa mara.
Kwa hiyo tumeendelea kuongeza uratibu ili kuhakikisha mazingira ya kufanya biashara Tanzania.
Yanapunguza urasimu lakini vile vile yanaendelea kuwa rafiki kwa wawekezaji rafiki kwa wafanyabiashara na rafiki hata kwa Watanzania wa kawaida ambao kila siku wanatamani kuendelea kufanya biashara.
Lakini vile vile tumeendelea kuboresha sera zetu ili kuongeza viwanda ambavyo ni vya manufacturing ambavyo kwa kiasi kikubwa vinasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuongeza pato la taifa, lakini vile vile kuongeza export kutoka nje.
Dodoma.
Naibu waziri wa wizara ya nishati, Mheshimiwa salome makamba ameitaka mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji ewura kuimarisha njia bora na ya haraka ya usafirishaji wa mafuta nchini ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa mafuta.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa nishati, makamba alipofanya kikao kazi na menejimenti ya mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji ewura mkoani Dodoma.
Moshimo makamba amesisitiza uwepo wa maghala ya kutosha kuhifadhia mafuta nchini ili wananchi waepukane na changamoto ya ukosefu wa mafuta na kupongeza jitihada za kukabiliana na changamoto hiyo ambayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuidhibiti.
Sambamba na hilo Mheshimiwa makamba ameitaka mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji ewura kuangalia namna bora ya upunguzaji gharama za vifaa vya uwekaji wa mifumo ya umeme majumbani ili kuongeza idadi ya watumiaji wa nishati hiyo hasa maeneo ya Vijijini.
Morogoro.
Wakulima wa miwa katika kijiji cha a chonde, wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wamegawiwa bure mbegu ya miwa aina ya r 570 ambayo inatajwa kuwa na uvumilivu wa ukame na magonjwa.
Daktari Catherine gwandu kutoka kituo cha utafiti wa kilimo, Watanzania tari amesema mradi huo wa uhimilivu wa maswala chakula unaofadhiliwa na serikali Jamhuri ya.
Gani Watanzania ni sehemu ya mikakati ya kuboresha kilimo cha miwa na kuinua kipato cha wakulima nchini.
Mkuu wa wilaya ya Kilombero, wakili msomi dastani kyobya amesema mbegu hiyo ya ara 570 kutoka hatari inaenda kuongeza kipato kwa wakulima wa wilaya yake huku akiwasisitiza wakulima kuendelea kulima kwa kuzingatia mbinu bora zinazotolewa na wataalamu wa kilimo.
Akimwakilisha mkurugenzi mkuu wa kituo cha utafiti wa kilimo wa Tanzania hatari dakta hii led hilde f litha msita amesema tayari inaendelea kufanya utafiti mbalimbali ili kuhakikisha wakulima wananufaika na shughuli za kilimo.
Pato hatari kibao anatuletea miwa ambao na sisi tuna kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa miwa ili tunayolima miwa yetu kuanzia kibaoni mpaka kule mswala station mpaka kidato na hapa hapa chonde kisawasawa tunakuwa na uwezo wa kuwa na kilimo chenye tija kwa kutumia mbegu nzuri ambayo ina mavuno mengi lakini eneo inakuwa chache zaidi kwenye utafiti wa mazao tunaanza utafiti wa udongo udongo upi unafaa kwa ajili ya kupanda mazao gani au kwa ajili ya kufanya shughuli gani za kilimo lakini pia mbegu tunavumbua aina mbalimbali za mbegu.
Ambazo zinajibu changamoto za wakulima.
Na kabla ya kuhitimisha habari za biashara na uchumi kutoka hapa shule ya fm tuangazie viwango vya kuuza na kununua fedha za kigeni siku hii ya leo.
Tuanzie pale nchini Marekani ambapo dola Marekani inanunuliwa kwa shilingi 2416 $0.28 na kuuzwa kwa shilingi 2440 $0.45.
Euro inanunuliwa kwa shilingi 2785 $0.73 na kuuzwa kwa shilingi 2813 $0.59.
Shilingi ya Kenya inanunuliwa kwa shilingi ya 18 $0.62 na kuuzwa kwa shilingi 18 $0.81 nayo shilingi ya Uganda inanunuliwa kwa shilingi 0 $0.66 na kuuzwa kwa shilingi 0 $0.67.
Mwisho wa habari za biashara na uchumi kutoka hapa show fm 97 nukta 3 megereza sauti ya Mungu unaungana nasi majira ya 07:00 kamili mchana kwa muhtasari wa habari.
Mimi ni William mmbando.
Yo-yo yo.
And the 97.3 Shalom FM.