Blog.

RadioOne - 2025-10-17T10:00:00.623Z

RadioOne

--:--
--:--

Transcription

Halo dada kaka yaani bora umenipigia huku na matatizo jamaa watu wengi kijijini saa hizi wanaumwa sana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza lakini hawawezi kumudu gharama zake na hapa hivi ninavyokwambia yule mjomba wa nanyamba kuleanaumwa.se dada hujasikia kama tukimchagua doctor samia suluhu hassan kuwa rahisi ndani ya siku 100 za kwanza serikali itagharamia matibabu ya saratani figo na sukari kwa wasiojiweza kaka kama ni hivyo kama sisi sasa tenki.

Kazi na utu tunasonga mbele chagua samia chagua ccm 10/29.

A.

Ikitangaza 1 kwa 1 kutoka mikocheni dar es Salaam.

Hii ni redio one msikilizaji kaa tayari kusikiliza taarifa hii ya habari.

Imetimia 07:00 kamili radio one inakuletea taarifa ya habari msomaji ni othuman Suleiman kwanza ni mukhtasari wake.

Makamu wa rais Mheshimiwa daktari philip mpango wa atamwakilisha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta samia suluhu hassan katika mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya bwana Raila Odinga.

Chama cha ACT wazalendo kimesema kikichaguliwa kuiongoza Zanzibar kupitia uchaguzi mkuu ujao, serikali yake itaandaa mpango maalum wa matumizi bora ya mbolea.

Matumizi bora ya mabonde yaliyopo visiwani humo ili kuongeza uzalishaji katika kilimo.

Polisi nchini Kenya imewaua kwa risasi watu wanne katika purukushani za kuwatawanya waombolezaji katika kuuaga mwili wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga katika uwanja wa michezo jijini Nairobi.

Uturuki mwatuma wataalamu kadhaa wa uokozi kwenda ukanda wa gaza kulisaidia kundi la hamas kuitafuta miili ya mateka wa Israel.

Tunaanza na habari za kitaifa dar es Salaam.

Makamu wa rais Mheshimiwa dokta philip isdori mipango yuko jijini Nairobi nchini Kenya kumwakilisha rais dokta samia suluhu hassan katika mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya bwana Raila Odinga.

Taarifa ya ofisi ya makamu wa rais imesema wengine waliopo katika msafara huu wa makamu wa rais ni pamoja na rais mstaafu wa awamu ya 4 Mheshimiwa jakaya Kikwete, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, balozi thabit mahmoud kombo.

Taarifa hiyo imesema mazishi ya marehemu Raila Odinga yanafanyika katika uwanja wa nyayo jijini Nairobi.

Mwanasiasa huyo maarufu nchini Kenya alifariki dunia juzi Jumatano nchini india ambako alikwenda kwa matibabu.

Bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe amin.

Pemba.

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT wazalendo Mheshimiwa othman masoud othman amesema chama hicho kikipata ridhaa kupitia uchaguzi mkuu yao.

Serikali yake itaandaa mpango maalum wa matumizi ya mabonde yaliyopo Unguja na pemba ili yatumike kwa tija katika uzalishaji.

Amesema hayo wakati akiwa huko shengejuu wilayani wete, jimbo la pandani Kaskazini Pemba alipozungumza na wakulima wa mashamba ya chumvi mwani mbogamboga na matikiti akiwa kwenye kampeni za uchaguzi wa 10/29 mwaka huu.

Amesema hatua hiyo itaongeza.

Kupanda.

Kupanga matumizi sahihi ya uzalishaji wenye tija katika mabonde hayo amesema licha ya kuwepo mabonde mengi yanayoweza kuzalisha vyema mabonde hayo hayatumiki kwa tija kwa kuwa wakulima na wazalishaji wengine wa mbogamboga hawawezeshwi ili walime na kuvuna kwa muda mrefu kama inavyofanyika katika nchi nyinginezo.

Mwanza serikali kupitia dira ya maendeleo ya mwaka 2025 2050 imepanga kuhakikisha taifa linakuwa na uhakika wa maji kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi linalo dumisha na kuendeleza uhifadhi wa ikolojia na mfumo imara na shirikishi wa usimamizi wa ardhi oevu, maji na rasilimali nyinginezo.

Mkurugenzi msaidizi wa huduma za maji bwana robert sunday amesema hayo katika uzinduzi wa bondia 8 bodi ya 8 yale bonde la ziwa Victoria na kuwataka wajumbe wa bodi hiyo wasitumie.

Wasimamie vyema mifumo yote iliyowekwa katika sekta ya maji mkuu wa mkoa wa Mwanza bwana said mtanda ameitaka bodi hiyo iwasaidie wananchi teknolojia ya uchimbaji visima ili kudhibiti uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uchimbaji holela.

Iringa.

Naibu katibu mkuu wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu, felister demo amesema wataalamu wa maendeleo ya jamii wana jukumu la msingi kuhakikisha kuwa jamii inaishi katika maadili na kuzingatia mila na desturi za Kitanzania zinazofaa.

Akizungumza katika chuo cha maendeleo ya jamii, ruaha amesema nidhamu katika jamii haipo tena na wimbi la mmomonyoko wa maadili limekuwa kubwa kwani vijana hawana hofu na na kutumia lugha zisizofaa hadharani hasa katika mitandao ya kijamii hata kwa watu waliowazidi umri.

Akimpongeza chuo hicho kwa kazi nzuri na ikifanya kwa kuwainua watoto wa kike na kuwajengea uwezo wa kujikomboa kiuchumi ikiwemo kushona cherahani na stadi nyingine za maisha.

Mkurugenzi wa maendeleo ya jamii kutoka wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum bwana Patrick golwike amesema serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha vyuo hivi vya kati vinatoa mafunzo stahiki na kuinufaisha jamii.

Unaendelea kusikiliza taarifa ya habari kutoka radio one zifuatazo sasa ni habari za kimataifa Nairobi.

Polisi nchini Kenya imewaua kwa risasi watu wanne katika purukushani za kuwatawanya waombolezaji katika kuuaga mwili wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga katika uwanja wa michezo jijini Nairobi.

Raila Odinga alikuwa kiongozi maarufu wa kisiasa katika nchi ya Kenya.

Kwa miongo kadhaa mfungwa wa zamani wa kisiasa na mgombea wa urais mara 5 bila mafanikio alifariki dunia.

Juzi Jumatano nchini india akiwa na umri wa miaka 80 machafuko yamezuka wakati umati mkubwa wa watu walipovamia na kuufungua mlango katika uwanja mkuu wa michezo wa Nairobi na kusababisha wanajeshi kufyatua risasi hewani.

Ankara.

Kutuma wataalamu kadhaa wa uokozi kwenda ukanda wa gaza ili kulisaidia kundi la hamas kuitafuta miili ya mateka ya Israel ambaye inaaminika wamefukiwa katika vifusi vya majengo yaliyoporomoshwa kwa vita tangazo la kutumwa kwa wataalamu hao limetolewa wakati asita ikiongezeka nchini Israel, hususan miongoni mwa familia za mateka baada ya hamas kusema imeshindwa kuipata miili ya ndugu na jamaa zao.

Familia hizo zimeitaka serikali Israel kusitisha utekelezaji wa hatua zinazofuata za mkataba wa kusitisha vita hadi pale ahamad itakapoikabili miili ya mateka.

19 waliopoteza maisha wakiwa kizuizini hamas imesema imedhamiria kutimiza matakwa ya mkataba uliosimamiwa na Marekani ikiwa ni pamoja na kuikabidhi miili yote ya mateka inapopatikana.

Viongozi wa Israel wametishia kuanzisha tena vita au kuzuia upelekwaji wa misaada ya ukanda wa ghasa iwapo miili hiyo haitapatikana kwa haraka.

New York.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Antonio guterres amelaani mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini madagascar baada ya wiki kadhaa za maandamano ya umma dhidi ya utawala wa rais andry rajoelina.

Bwana guterres amekosoa mabadiliko ya uongozi yasiyozingatia katiba na ametoa wito wa kurejea kwa utawala wa kiraia nchini humo chini ya misingi ya kikatiba.

Matamshi hayo ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa yanakuja wakati canal Michael andrew nina leo anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa taifa hilo hafla itakayofanyika katika majengo ya mahakama ya juu ya kikatiba.

Kwenye mji mkuu wa taifa hilo antananarivo Umoja wa mataifa pia umelaani mapinduzi hayo na kuisimamisha madagascar katika uanachama wake.

Wakulima.

Rais mpya wa peru jose jerry amepuuza shinikizo linalomtaka ajiuzulu kufuatia kifo cha mwandamanaji kilichotokea wakati wa maandamano yalioyoongozwa na vijana dhidi ya serikali ya nchi hiyo.

Amesema ataachia madaraka na badala yake ataendelea kutekeleza majukumu yake na kurejesha uthabiti katika taifa hilo kuendesha mashtaka wamefungua uchunguzi wa kifo cha mwandamanaji mwenye umri wa miaka 30 na miwili ambaye taarifa zimesema alipigwa risasi na polisi wa kutuliza ghasia maelfu ya vijana wa peru wameandamana kwa karibu mwezi mzima kudai malipo mazuri ya mishahara na kuonyesha hasira dhidi ya vitendo vya uhalifu na madai ya rushwa iliyokithiri serikalini.

Kwa kukamilisha taarifa ya habari huo tena ni muhtasari wake.

Makamu wa rais Mheshimiwa dokta, philip isdori mpango atamwakilisha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta samia suluhu hassan katika mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga.

Chama cha ACT wazalendo kimesema kikichaguliwa kuiongoza Zanzibar kupitia uchaguzi mkuu yao, serikali yake itaandaa mpango maalum wa matumizi bora ya mabonde yaliyopo visiwani humo ili kuongeza uzalishaji katika kilimo.

Polisi nchini Kenya imeua watu wanne katika purukushani za kuwatawanya waombolezaji wakati wa kuuaga mwili wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga katika uwanja wa michezo jijini Nairobi na Uturuki mwatuma wataalamu kadhaa wa uokozi kwenda ukanda wa gaza ili kulisaidia kundi la hamas kuitafuta miili ya mateka wa Israel na huo ndio mwisho wa taarifa ya habari kutoka redio one 08:00 kamili unasomewa habari za saa na kwa taarifa nyingine ya habari usikose kujiunga nasi mikapo 02:00 kamili usiku.

Tanzania, zile favre radio station.

Yeah.

Yeah.

Hivi sasa ni 07:08.