Safina Radio - 2025-10-17T10:00:00.557Z
Safina Radio
Arusha
Transcription
Sadaka ya kujenga daraja la mafanikio daraja la kupata watoto daraja la ku la la kufanya biashara nifanikiwe daraja la duka langu hili ni daraja la watoto wangu.
Nataka nikuambie mambo yatatokea tena si siku nyingi mwana wa Mungu upate kuelewa mambo haya na tutazidi kuyafundisha zaidi kwa sababu ni ya muhimu sana katika maisha yako.
Mungu akubaliki sana na Mungu akutunze.
The.
Ni 01:00 na dakika ni 07:01 mchana ifuatayo ni taarifa ya habari kutoka redio safi na msomaji ni zaidi elias lebo ina kwanza ni muhtasari wake.
Mahakama kuu kanda ya tanga imewahukumu hamisi mkufya mwenye umri wa miaka 22 na Abdallah sebo mwenye umri wa miaka 20 kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kulawiti msichana mwenye umri wa miaka 16, mkazi wa mikunduni mkoani humo.
Jamii imetakiwa kuwa na tabia ya kwenda mara kwa mara kwenye kliniki maalum ili kujua hali za afya zao kutokana na kuongezeka kwa changamoto ya afya ya akili nchini.
Mwili wa kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga unaagwa kitaifa wakati huu katika ibada maalum mjini Nairobi ambayo imehudhuriwa na viongozi wakuu wa serikali mbalimbali duniani.
Habari kamili tunaanza na habari za kitaifa.
Tanga.
Mahakama hako kanda ya tanga imewahukumu hamisi jamali mkofia mwenye umri wa miaka 22 na Abdallah sebo mwenye umri wa miaka 20 wakaazi wa mbugani kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kulawiti msichana mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa mikumi mikanjuni mkoani humo.
Tukio hilo lililotokea mnamo 23.
26 Disemba 2023 katika eneo la mikanjuni, wilaya ya Tanga na baada ya tukio taarifa ziliripotiwa kituo cha polisi tanga, watuhumiwa walikamatwa na upelelezi kuanza mara 1.
Mnamo Disemba 27, 2023, watuhumiwa walifikishwa mahakama ya wilaya ya tanga kujibu kesi ya jinai na baada ya ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka kusikilizwa mnamo jana 10/16 mahakama iliwakuta watuhumiwa wote na hatia na kuwahukumu kifungo cha maisha jela.
Uamuzi huu unatafsiriwa kama hatua ya kuweka mfano kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na kulinda haki za waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia.
Arusha.
Mtaalamu wa afya ya akili kutoka halmashauri ya wilaya ya Arusha, dokta pascal pangilia ameiasa jamii kuwa na tabia ya kwenda mara kwa mara kwenye kliniki maalum ili kujua hali za afya zao kutokana na kuongezeka kwa changamoto ya afya ya akili.
Doctor kayiraya ameyasema hayo jijini Arusha wakati wa kufungua semina juu ya umuhimu wa kutunza afya ya akili kwa baadhi ya watumishi.
Amesema kutokana na mtindo wa maisha wa sasa, ipo haja ya kuendelea kuikumbusha jamii kila kukicha kwa namna tofauti ili kuweza kupambana na wimbi hili la changamoto ya afya ya akili.
Ukweli ni kwamba jamii ya Watanzania inayoelezwa mzuri kuhusu afya ya akili na watu wanapitia changamoto nyingi sana.
Watu wanapitia misongo mingi uwezo wa kubeba hisia watu wengi hawana kutokana namna walivyozaliwa vitu walivyo berithi ni na changamoto wanazopitia kila siku kwa tumekuwa tukishuhudia watu wengi wanatumia pombe sana vile wesho na mazingira ya kupambana na hali wanayopitia na wengi wanaopitia changamoto hawaji kwa ajili ya tiba wanachelewa sana wakitokea wamekuja wanakuja muda umeenda na ikiwa tayari walishakuwa na madhara makubwa.
Watu ambao wanasherehekea shida kwenye familia zao.
Kwa hiyo mafunzo haya yameleta msawazo mzuri kuhamasisha jamii kuhusu maswala ya afya ya akili kupata huduma mapema utulivu wa akili dar es Salaam.
Serikali kupitia maabara ya taifa ya afya ya jamii imejipanga kuimarisha ufuatiliaji na kuwajengea uwezo wataalam wa afya nchini ili kuboresha utambuzi wa haraka wa ugonjwa wa kipindupindu hatua itakayosaidia kudhibiti kabla hauja sambaa.
Akizungumza jijini dar es Salaam wakati wa kikao cha tathmini ya utekelezaji wa miaka miwili ya mradi wa kujenga uwezo maabara ya taifa ya afya ya jamii unaofadhiliwa na shirika la korea Foundation for International healthcare.
Kaimu mkurugenzi wa maabara hiyo bwana ambele mwafo fulango amesema mpango wa mwaka wa 3 wa mradi huo umejikita katika kujenga uwezo wa wataalamu katika maeneo mbalimbali nchini.
Tumekubaliana kauli 1 kwamba tufanye ufuatiliaji au tuboreshe au utambuzi wa ugonjwa wa kipindupindu ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa ambao umekuwa ukiripotiwa mara kwa mara sehemu mbalimbali unatokea huku natokea huwa hakuna sehemu 1 ambayo tunasema kwamba haiko salama sana au sehemu.
Mengine ambayo iko haiko sawa sana ndio maana hata huu mradi sasa hivi ndivyo kwenda unatoka nje ya dar es Salaam.
Kwa hiyo tutakwenda kwenye mikoa sio dar es Salaam tutakwenda na mikoa mingine nchini kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunajenga uwezo wa wataalam kwa kuweza kutambua kwa haraka kama kumekuwa na ugonjwa wa kipindupindu.
Iringa.
Imeelezwa kuwa wataalamu wa maendeleo ya jamii wana jukumu la msingi la kuhakikisha kuwa jamii inaishi katika maadili ikiwemo kuzingatia mila na desturi za Kitanzania zinazofaa.
Hayo yamebainishwa na naibu katibu mkuu wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, felister mdemu alipotembelea chuo cha maendeleo ya jamii ruaha mkoani Iringa.
Felista ameeleza kuwa nidhamu katika jamii haipo tena na wimbi la mmomonyoko wa maadili limekuwa kubwa kwani vijana hawana hofu ya kutumia lugha zisizofaa hadharani na kwenye mitandao ya kijamii hata kwa watu waliowazidi umri.
Naye mkurugenzi wa maendeleo ya jamii kutoka wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Patrick golwike amesema kutokana na maadili kushuka wataalamu wa maendeleo ya jamii wana jukumu la kufanya tafiti na kuja na majibu yenye suluhisho ili kutokomeza mmomonyoko wa maadili.
Unaendelea kusikiliza taarifa ya habari kutoka redio safina zifuatazo sasa ni habari za kimataifa.
Nairobi.
Mwili wa kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga unaagwa kitaifa wakati huu katika ibada maalum mjini Nairobi ambayo imehudhuriwa na viongozi wakuu na wawakilishi wa serikali mbalimbali duniani.
Ibada hiyo inaendelea muda huu kwenye uwanja wa michezo wa nyayo na ikiongozwa na rais wa nchi hiyo, William Ruto.
Odinga wanasiasa kigogo upinzani aliaga dunia siku ya Jumatano akiwa nchini india alikokwenda kwa matibabu na mwili wake ulirejeshwa nyumbani jana Alhamisi na maelfu ya watu walipata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kwenye uwanja wa kasarani nje kidogo ya mji mkuu Nairobi.
Hata hivyo, zoezi hilo lilikumbwa na vurumai iliyosababisha vifo vya watu wasiopungua watatu baada ya polisi kufyatua risasi ili kuwatawanya waombolezaji waliokuwa wakisongamana kuelekea jukwaa la watu mashuhuri.
New York.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Antonio guterres amelaani mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini madagascar baada ya wiki kadhaa za maandamano ya umma dhidi ya utawala wa rais andry rajoelina.
Guterres amekosoa mabadiliko ya uongozi yasiyozingatia katiba na ametoa mwito kwa kurejea kwa utawala wa kiraia nchini ya misingi ya katiba.
Matamshi yake ameyatoa wakati kanali wa jeshi aliyechukua madaraka siku ya Jumanne Michael randy rina anatarajiwa kuapishwa leo ijumaa kuwa rais wakati wa hafla itakayofanyika katika majengo ya mahakama ya juu ya katiba kwenye mji mkuu antananarivo.
Na hatimaye ni ilima.
Rais mpya wa peru jose jerry amepuuza miito na shinikizo la kumtaka ajiuzulu kufuatia kifo cha mwandamanaji mmoja kilichotokea wakati wa wimbi kubwa la maandamano yanayoongozwa na vijana dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
Kiongozi huyo amesema hatawaachia madaraka na kwamba ataendelea kutekeleza majukumu yake ya kurejesha udhibiti kwenye taifa hilo la Amerika ya kusini.
Maelfu ya vijana wa peru wameing.