Radio Kwizera - 2025-10-17T13:00:00.585Z
Radio Kwizera
Ngara
Significant Highlights
2 HighlightsThese are the most relevant segments extracted from this record based on semantic analysis.
Transcription
10 kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki sawa na 09:00 kamili alasiri kwa saa za Afrika ya kati leo ni ijumaa ya 10/17 mwaka 2025 hujambo msikilizaji na huu ni wasaa wa mseto leo na kwanza tunaanza na makala ya duru zetu alasiri inakuletea dakika 30 za habari uchambuzi, uchumi na biashara na michezo na burudani uko nami pasience scarion tulio nayo alasiri ya leo.
Serikali imetangaza kima cha chini cha mshahara wa sekta binafsi kutoka shilingi laki 2, 75,060 hadi shilingi laki 3 58,322 ikiwa ni ongezeko la 33/100 nukta 4.
Benki kuu ya Tanzania bot imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa taasisi hiyo inachapisha fedha na kuzisambaza kwa ajili ya kugharamikia uchaguzi.
Na serikali ya Burundi imetangaza mpango wa kuanzisha mradi wa kadi ya bima ya afya ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za matibabu bila changamoto.
Tuma maoni yako kwa taarifa utakazo zisikiliza katika makala hii kupitia namba 0692573615 ukitueleza nini maoni yako juu ya taarifa hizi na ujumbe wake utasomwa hapo baadaye, lakini pia msikilizaji unaweza kutufuatilia youtube kwa kuandika kwizera tv na katika ukurasa wa Facebook wa radio kwizera tupo mubashara.
Tuanze na duru habari na zawadi bashemela karibu sana zawadi asante asante sana pasience serikali imetangaza kima cha chini cha mshahara wa sekta binafsi kutoka shilingi laki 2 75,060 hadi shilingi laki 3 58,322 ikiwa ni ongezeko la 33/100 nukta 4.
Akitangaza kima hicho cha sekta binafsi leo waziri wa.
Nchi ofisi ya waziri mkuu, kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu ridhiwani Kikwete amesema kuongezwa kwa kima cha mshahara ni takwa la kisheria.
Kwa mujibu wa waziri ridhiwani, mapitio ya kima cha chini cha mshahara hufanyika kila baada ya miaka mitatu ambapo tangazo la mwisho lilitolewa mwaka 2022.
Ameeleza kuwa serikali inataka waajiri wote wa sekta binafsi kuhakikisha wanazingatia na kutekeleza kima hicho kipya.
Cha mshahara kwa mujibu wa sheria amri ya kima cha chini cha mshahara imegusa sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo, sekta ya afya, sekta ya mawasiliano, sekta ya usafirishaji, sekta ya hoteli, sekta ya madini, biashara na viwanda, shule binafsi, huduma za ulinzi binafsi ni shati, uvuvi, huduma za baharini, michezo, utamaduni pamoja na huduma nyinginezo.
Aidha, kwa mujibu wa amri hiyo, kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi kitaanza kutumika rasmi tarehe 1 Januari mwaka 2026, ameonya kuwa ofisi yake.
Na haitasita kuchukua hatua kwa waajiri watakaokaidi au kushindwa kutekeleza agizo hilo kwa makusudi.
Akisisitiza kuwa serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wake.
Benki kuu ya Tanzania BOT imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa taasisi hiyo inachapisha fedha na kuzisambaza kwa ajili ya kugharamia uchaguzi jambo linalosababisha hofu kwa baadhi ya wananchi ambao wameanza kutoa fedha zao katika benki za biashara.
Gavana wa benki kuu, Emmanuel tutuba amesema taarifa hizo si za kweli na zimekusudiwa kupotesha kupotosha umma.
Amesema benki kuu ya Tanzania.
Inachapisha fedha kwa mujibu wa sheria na kanuni kwa kuzingatia mzunguko wa uchumi na mahitaji ya kubadilisha fedha chakavu na si kwa sababu ya uchaguzi kama inavyodaiwa.
Aidha amebainisha kuwa sera za fedha zimeendelea kutekelezwa kwa ufanisi ili kudhibiti matukio ili kudhibiti mfumuko wa bei ambapo wastani wake umebaki katika kiwango cha 3/100 nukta 3 katika kipindi cha miezi 10 hadi Septemba mwaka huu.
Gavana tutuba amewahakikishia wananchi kuwa benki zote nchini zipo katika hali nzuri ya kifedha.
Zikiwa na mitaji ya kutosha na ukwasi wa kuridhisha huku mifumo ya malipo ikiendelea kufanya kazi kwa ufanisi wakulima wilayani muleba mkoani Kagera wametakiwa kuzingatia mbinu bora za kilimo katika msimu huu wa kilimo ulioanza rasmi mwezi Oktoba ili kuongeza uzalishaji na kupata mazao mengi na bora.
Afisa kilimo wa wilaya ya muleba bwana joseph seni amesema wakati huu wakulima hutumia kikamilifu mvua zilizoanza kunyesha kwa kukamilisha maandalizi ya mashamba.
Na kutumia mbegu bora aidha, bwana seni amewataka wakulima kushirikiana na maafisa ugani waliopo kwenye kata na vijiji ili kupata mafunzo na usaidizi wa kitaalam utakaowasaidia kuongeza tija mashambani ili kuondokana na changamoto kulima kilimo cha mazoea baada ya kutoka kwenye utabiri huyo alisema wiki ya kwanza na wiki ya pili tutakuwa na mvua zitaanza kuonyesha mvua za vuli kwa maana ambazo zitakuwa juu ya wastani na wastani na sasa kweli zimeanza kunyesha.
Kwa hiyo sasa ni vizuri wakulima sasa tunawashauri waanze kuzitumia mvua hizi.
Kwa usahihi kwa sababu hatutakuwa na mvua nyingi kwa sasa wakamilishe uandaaji wa mashamba kwa wale ambao walikuwa wamechelewa na kuanza upandaji kwa kutumia mbegu bora na pembejeo bora zinazopatikana kwenye maeneo yetu.
Baadhi ya wakulima wameomba maafisa ugani kuendelea kutoa elimu kwenye maeneo yao badala ya kukaa ofisini katika kipindi hiki cha maandalizi kutokana na baadhi yao hawana elimu yoyote ya kilimo bora.
Yeah.
Serikali ya Burundi imetangaza mpango wa kuanzisha mradi wa kadi ya bima ya afya inayojulikana kama cam ambayo inalenga kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za matibabu bila changamoto.
Akizungumza kuhusu mpango huo, katibu mkuu wa wizara ya afya nchini Burundi, doctor oscar ntihabose amesema kadi hiyo itawaunganisha wananchi wote katika taasisi 1 ya bima jambo litakalowezesha huduma za matibabu kutolewa kwa urahisi na ufanisi zaidi.
Aidha doctor ntihabose ameeleza kuwa hatua hiyo inakuja kufuatia malalamiko ya wananchi kutoka mikoa mbalimbali nchini humo kuhusu changamoto za upatikanaji wa huduma za afya ikiwemo ongezeko la bei ya dawa katika vituo vya afya na hospitali.
Amesisitiza kuwa serikali inatambua ugumu wanaoupata familia zenye kipato cha chini katika kupata huduma za matibabu na ndio maana imeamua kuweka mfumo huo wa bima ya afya ili kupunguza mzigo kwa wananchi.
Na watu wawili wamefariki na wengine watatu wamejeruhiwa kwa risasi wakati wa mashambulizi kati ya makundi mawili ya wazalendo kwenye vijiji vya runinga na luvungi, tarafa ya uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, kiongozi wa shirika la raia katika tarafa ya uvira, bwana kidumu frelimo amesema hali ya kutoelewana kati ya kundi la jenerali Nyerere na kundi la jenerali makanaka ki imeripotiwa jana jioni hali iliyosababisha kurushiana.
Risasi kati yao amesema waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu kwenye hospitali kuu ya mji wa uvira, mashirika ya kutetea haki za binadamu katika tarafa ya uvira ya amelaani mauaji hayo na kuomba serikali kuingilia kati hasa kwa kufikisha kwenye vyombo vya sheria.
Wazalendo waliohusika na vurugu hizo kwani raia wamepata wasiwasi na wengine wamehama vijiji vyao uwanza wazua.
Msikilizaji kila mshangao wa leo ni hadithi ya kesho huanza wazua na huo ndio mwisho wa duru habari jioni ya leo endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii Instagram tik tok na x atyo radio kwizera fm youtube.