Radio Maria Tanzania - 2025-12-17T10:00:00.612Z
Radio Maria Tanzania
Dar es Salaam
Transcription
Msikilizaji mpenzi wa radio maria kaa tayari kusikiliza taarifa ya habari kutoka tbc.
Hivi sasa ni 07:00 kamili.
Hii ni taarifa ya habari kutoka tbc taifa msomaji betty tesha kwanza muhtasari wake.
Wakala wa barabara nchini tanroads na wakala wa barabara za mijini na Vijijini, tarura wametakiwa kufanya sensa na tathmini ya fedha za miradi ya ujenzi wa barabara ili kuwabana wakandarasi wanaoshindwa kutekeleza miradi kulingana na mikataba waliosaini.
Taasisi ya moyo jakaya Kikwete imesaini makubaliano ya uendeshaji wa hospitali ya Arusha lutheran Medical centre maarufu kwa jina la seliani kwa kipindi cha miaka 20 ijayo ili kuleta huduma za kibingwa karibu na wananchi.
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imemfutia kesi na kumwachia huru irene m abeche aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya uhaini baada ya mkurugenzi wa mashtaka nchini dpp kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi na mashtaka dhidi yake.
Venezuela imetuma rasmi malalamiko yake kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa juu ya kile inachokiita wizi wa Marekani iliyoteka meli yake ya mafuta kwenye Bahari ya caribbean wiki iliyopita.
Habari kamili.
Songwe.
Waziri mkuu doctor mwigulu nchemba ameutaka wakala wa barabara nchini tanroads na wakala wa barabara za mijini na Vijijini, tarura zifanye sensa na tathmini ya fedha za miradi ya ujenzi wa barabara ili kuwabana wakandarasi ambao wanashindwa kutekeleza miradi kulingana na mikataba waliosaini huku fedha za serikali zikipotea.
Akizungumza mjini tunduma mkoani Songwe, doctor nchemba amesema watendaji wa umma hasa katika taasisi hizo wanawajibika kuwa na nidhamu hasa katika makuu dhibiti wakandarasi.
Ambao hawatekelezi miradi waliopewa huku wakisababisha kero kwa wananchi na hasara kwa serikali akielezea uadilifu kwa wakandarasi, waziri mkuu ameitaka wakandarasi hao walipwe malipo yao kwa kutumia akaunti za ndani na sio nje ya nchi ili kuepuka wakandarasi matapeli huku akihimiza wakandarasi wazawa kupewa zabuni za ujenzi.
Waziri mkuu pia amehimiza wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu huku akisisitiza kwamba mpango wa bima ya afya kwa wote.
Utaanza kutekelezwa Januari mwakani.
Arusha.
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya moyo ya jakaya Kikwete jk CI doctor peter kisenge amewataka wafanyakazi wa hospitali ya Arusha lutheran Medical centre maarufu kwa jina la seliani ya mjini Arusha kufanya kazi kwa bidii kujituma na kuzingatia maadili ya kazi ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi dokta kisenge ametoa wito huo jijini Arusha wakati akizungumza na wafanyakazi hao baada ya hospitali hiyo kusaini makubaliano ya uendeshaji na taasisi ya moyo ya jakaya Kikwete.
Kwa kipindi cha miaka 20 ijayo ili kuleta huduma za kibingwa karibu na wananchi.
Utekelezaji rasmi wa mkataba huo utaanza rasmi Januari mosi mwakani kwa kambi kubwa ya kuwapima wananchi magonjwa ya moyo.
Lengo likiwa ni kuwafikishia wananchi huduma za kibingwa karibu badala ya kutumia gharama kubwa kuzifuata jijini dar es Salaam.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa seliani, doctor godwin kivuyo amesema makubaliano hayo yamekuja baada ya hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kkkt dayosisi ya Kaskazini kati.
Huomba kuingia ubia na serikali mwaka 2023 na kufikia makubaliano mwaka 2025.
Dar es Salaam.
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imemfutia kesi na kumwachia huru mshtakiwa irene mabechi aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya uhaini baada ya mkurugenzi wa mashtaka nchini dpp kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi na mashitaka dhidi yake.
Uamuzi huo umetolewa na hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, hassan makube baada ya wakili wa serikali, erick davis kuieleza mahakama kwamba ofisi ya dpp amewasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi na mashitaka.
Dhidi ya mshtakiwa irene alikabiliwa na kesi ya uhaini tukio analodaiwa kutenda 10/29 mwaka huu katika jiji la dar es Salaam ambapo alidaiwa kwa nyakati tofauti kati ya Aprili mosi na 10/29 alikula njama za kutenda kosa la uhaini ikiwemo kuinua kunuia kuzu.
Ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 usifanyike.
Tanga.
Rais dokta samia suluhu hassan ameipongeza kamati ya pamoja ya wataalam wa uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya kwa kuhakikisha mpaka unaotenganisha nchi hizo 2 unaimarishwa rais samia ametoa pongezi hizo baada ya kupatiwa taarifa na mkuu wa mkoa wa tanga, balozi doctor batilda buriani kuhusu uwepo wa kikao cha kamati ya pamoja kinachojumuisha timu za wataalam kutoka Tanzania na Kenya walipofika mkoani.
Tanga tarehe 15 mwezi Disemba na kuelezwa uwepo wa kikao hicho akizindua rasmi kikao hicho cha siku 5 kinachoendelea mkoani humo.
Mkuu wa mkoa huo, dokta buriani amesema rais samia ameridhishwa na taarifa za utekelezaji wa kazi hiyo na kuwataka wataalam kuitumia nafasi hiyo kufanya kazi kwa weledi.
Dodoma.
Wadau wa sekta ya kilimo wametakiwa kubuni mbinu endelevu za kuboresha uzalishaji wa zao la alizeti ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya kupikia na kuimarisha uchumi wa wakulima.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, rosemary senyamule ametoa rai hiyo jijini Dodoma katika kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya kilimo kwa lengo la kutathmini namna ya kuboresha upatikanaji na uzalishaji wa zao hilo unaendelea kusikiliza taarifa ya habari kutoka.
Tbc taifa.
Nairobi.
Serikali ya kaunti ya Nairobi nchini Kenya imeidhinisha rasmi utaratibu wa kutoa siku 2 kila mwezi za kupumzika kwa sababu ya hedhi kwa wanawake wafanyakazi kama sehemu ya mfumo wa rasilimali watu wa kaunti hiyo.
Uamuzi huu umefikiwa baada ya kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na gavana wa jimbo hilo, Johnson sakaja kilichopendekezwa kuingiza usaidizi wa afya ya hedhi katika sera ya rasilimali watu kwa lengo la kuboresha ustawi wa wafanyakazi na kuongeza utendakazi.
Kwa wanawake kazini taarifa ya kaunti inabainisha kuwa changamoto za afya ya hedhi hususan maumivu makali ya hedhi huathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wa wanawake na utendaji wao kazini.
Tafiti zinaonyesha kuwa kati ya wanawake 60 na watano hadi 80 kwa mia hukabiliwa na maumivu ya hedhi na idadi kubwa ufanisi wao kazini huathirika zaidi.
Mbeya.
Baadhi ya wananchi mkoani mbeya wameiomba serikali kupitia wizara ya maji kuharakisha mradi wa maji wa mto kiwira utakaoenda kutatua changamoto ya haraka ya maji katika sehemu zao kutokana na mgao na ukosefu wa maji uliopo.
Wakizungumza na tbc jijini mbeya, wananchi hao kutoka kata ya isanga na maeneo ya pembezoni mwa jiji hilo wameeleza jinsi wanavyopata changamoto ya maji huku wakiiomba serikali iwatatulie changamoto hiyo kuharakisha mradi mkubwa wa maji.
Unaoendelea kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji mbeya, mhandisi barnabas konga amesema ucheleweshwaji wa mradi huo unatokana na baadhi ya watu kushindwa kulipwa fidia zaidi ya shilingi bilioni 2 kwa wakati.
Amesema wao kama mamlaka watahakikisha kila mwananchi aliyepatiwa aliyepitiwa na mradi huo wa maji analipwa fidia.
Porto novo.
Mahakama ya uhalifu wa kiuchumi na ugaidi nchini benin muwashitaki watu wapatao 30 wengi wao wakiwa wanajeshi kwa jaribio la mapinduzi lililoshindwa mapema mwezi huu.
Vyanzo vya mahakama vinasema watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa uhalifu, mauaji na kuhatarisha usalama wa taifa.
Wanajeshi wa ngazi za chini walijitokeza kwenye televisheni ya taifa hilo 12/07 mwaka huu na kutangaza kuipindua serikali ya rais patrice talon.
Lakini jaribio hilo lilizimwa haraka na wanajeshi watiifu kwa msaada wa kikosi cha anga cha Nigeria na kikosi maalum cha Ufaransa.
Caracas.
Venezuela imetuma mali.