FADECO Community Radio - 2025-10-14T17:00:00.488Z
FADECO Community Radio
Bukoba
Transcription
Kuwa rais dokta philip mpango amesema Watanzania wanao wajibu wa kulinda uhuru wa taifa.
Kuimarisha mshikamano na umoja pamoja na kulinda maadili.
Watanzania wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu ikiwa ni sehemu ya kumuenzi baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Viongozi wa vyama vya siasa nchini wameendelea na kampeni za kunadi sera za vyama vyao.
Katika maeneo mbalimbali nchini na kuomba kura.
Shirika la fedha la kimataifa IMF limempongeza rais samia suluhu hassan.
Kwa kusimamia vyema sera za uchumi na fedha za nchi yake ikiwemo kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei.
Habari kamili, mbeya.
Makamu wa rais, daktari philip mpango ametaja mambo manne ambayo Watanzania wanapaswa kuendelea kumuenzi kwa vitendo.
Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Akizungumza katika kilele cha mbio za mwenge wa uhuru zilizofanyika mkoani mbeya.
Dokta mpango amesema Watanzania wana wajibu wa kulinda uhuru wa taifa kujenga na kuimarisha mshikamano na Umoja wa kitaifa kulinda maadili ya Mtanzania na kuhifadhi mazingira.
Amesema serikali itaendelea kuratibu na kuenzi yale yote ambayo baba wa taifa aliweka misingi ya taifa katika nyanja za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kidiplomasia.
Makamu wa rais pamoja na mambo mengine amezindua kitabu cha miaka 60 historia ya mwingi uhuru tangu nimeanza kukimbizwa nchini kilichoandikwa na Watanzania wazalendo.
Akitambulisha kitabu hicho waziri mkuu, kassim majaliwa.
Amemhakikishia makamu wa rais kuwa kitabu hicho kimeeleza tunu hiyo muhimu ya mwenge wa uhuru ambayo imekuwa na mafanikio makubwa katika nchi.
Morogoro.
Viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kkkt dayosisi ya Morogoro umehimiza vijana nchini kuenzi na kuishi kwa vitendo falsafa za baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kulinda na kudumisha amani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika maadhimisho ya kumbukizi ya kifo cha baba wa taifa, viongozi hao wamesisitiza kwamba vijana wanalo jukumu la msingi la kuhakikisha taifa linakuwa na mshikamano na kuacha kutumiwa vibaya na wanasiasa wenye lengo la kuvuruga amani ya nchi.
Aidha, amewataka vijana kuhakikisha wanashiriki katika uchaguzi kwani maamuzi yao ndio mbegu inayoweza kuleta nuru ya matumaini kwa Watanzania wote kwa ujumla.
Dar es Salaam.
Watanzania wamehimizwa kujitokeza kwa wingi ka kwa amani na utulivu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika 10/29 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kumuenzi baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakizungumza wakati wa kongamano walioambukizwa miaka 26, kifo cha baba wa taifa baadhi ya wakaazi wa dar es Salaam wamesema ili kumuenzi baba wa taifa, Watanzania wanapaswa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa 10/29 mwaka huu.
Na washiriki wa kongamano hilo ambao ni viongozi wastaafu wamesisitiza umuhimu wa kudumisha amani mshikamano na kutumia haki ya Kidemokrasia kwa kushiriki uchaguzi mkuu huku mkoani Arusha.
Watanzania wamehimizwa kuendelea kuenzi lugha ya Kiswahili iliyotumika kuwaunganisha wakati wa ukombozi licha ya kuwa na zaidi ya makabila mengi hapa nchini jambo ambalo limeacha alama.
Hadi sasa mhifadhi kiongozi wa makumbusho ya elimu viumbe bora akonaay amesema historia ya baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Alitumia lugha ya Kiswahili kuwaunganisha Watanzania na hata nchi jirani ambazo zimekuwa ziki tamani kujifunza.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia 10/14 mwaka 1999 anakumbukwa kutokana na uongozi wake thabiti wa kutetea haki za Watanzania na bara la Afrika kwa ujumla.
Zanzibar.
Mgombea urais Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi ccm dakta Hussein ali mwinyi.
Amesema endapo chama hicho kitapata ridhaa kwa mara nyingine serikali yake itahakikisha inaunda tume ya kuwahakiki fidia.
Kuhamishwa kwenye maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mgombea huyo wa urais Zanzibar kupitia ccm amesema hayo dimani wilaya ya magharibi b mkoa wa Mjini Magharibi katika mwendelezo wa kampeni zake ambapo amesema atahakikisha wananchi wote wanaodai fidia hawadhulumiwi na wanalipwa fidia zao kwa wakati kuhusu sekta ya uvuvi.
Mgombea huyo urais Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi ccm dakta Hussein ali mwinyi amesema atahakikisha serikali yake itaendelea kudhibiti uvuvi haramu.
Baada ya kulinda mazalia ya samaki, mgombea huyo wa urais Zanzibar kupitia ccmamesema.se.
Na hali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya inayochochea ustawi wa jamii.
Shinyanga.
Chama cha nld kimeahidi kuhakikisha mikataba yote ya madini baina ya serikali na wawekezaji inawanufaisha Watanzania ili wazawa wanufaike na utajiri wa rasilimali zilizopo nchini.
Ahadi hiyo imetolewa na mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho doyo, hassan doyo wakati akiendelea na kampeni zake wilayani kahama mkoani Shinyanga.
Aidha duru ameahidi kujenga soko la kisasa mjini kahama ili kuinua uchumi wa wananchi na kuongeza thamani ya mazao.
Kwa upande wake mgombea wa urais kupitia chama cha wakulima.
Psp kumjenga mali mwiru amesema akichaguliwa kuwa rais katika uchaguzi utakaofanyika 10/29 atatoa bima ya afya bure kwa wananchi wote nchini kwa kuwa afya ya mtu sio majaribio.
Meru amesema hayo wakati wa kampeni za chama chake zilizofanyika katika eneo la satellite mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani geita mkoani geita mwiru ameahidi kuwa atahakikisha huduma za afya katika vituo vya afya zitatoa huduma 20:04 na kusisitiza kujenga miundo mbinu barabara ili wakulima wasafirishe mazao yao.
Unaendelea kusikiliza taarifa ya habari kutoka tbc taifa.
Singida.
Mgombea mwenza wa urais wa chama cha mapinduzi ccm, balozi daktari Emmanuel nchimbi amesema endapo chama hicho kitapata ridhaa ya kuchaguliwa kuiongoza serikali kitahakikisha kinaendelea kuenzi falsafa za hayati baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere zilizojikita katika misingi ya amani, umoja na mshikamano.
Balozi daktari nchimbi amesema hayo alipokuwa akinadi sera za ccm katika kijiji cha ishenga jimbo la mkalama mkoani Singida ambapo amesema Watanzania watafanya kosa kubwa endapo wataacha misingi iliyoasisiwa na baba wa taifa.
Ambao pia anaenziwa na mgombea wa urais wa chama hicho, samia suluhu hassan amesema ndani ya miaka mitano ijayo serikali ya ccm itaimarisha sekta ya huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kujenga vituo vitano vya afya, zahanati 8 pamoja na nyumba 12 za wataalam wa afya katika jimbo hilo la mkalama.
Ameongeza kuwa serikali yasitisha hiyo itahakikisha mradi wa maji safi na salama wa ziwa Victoria unaendelea kutekelezwa katika jimbo la mkalama na iramba mashariki unakamilika.
Washington, DC Shirika.
Zile fedha la kimataifa IMF limempongeza rais samia suluhu hassan kwa kusimamia vyema sera za uchumi na fedha za nchi yake ikiwemo kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na namna anavyosimamia fedha za miradi zinazotolewa na taasisi hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Yameandaliwa ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika.
Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti na mkurugenzi mtendaji wa IMF anayesimamia idara ya Afrika abebe selasi na mkurugenzi mtendaji wa kundi la kwanza la nchi za Afrika wa ushirika hilo.
Adrian ubisi walipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki mikutano ya mwaka ya shirika la fedha la kimataifa IMF na benki ya dunia jijini Washington dc nchini Marekani.
Maafisa hao wa IMF wamesema Tanzania ni nchi ya mfano katika usimamizi wa sera za uchumi wa fedha ambapo licha ya changamoto za uvikwe 19 na mizozo ya kisiasa inayoendelea sehemu mbalimbali duniani, tathmini ya shirika hilo inaonyesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi.
Za Afrika.
Akizungumza katika mkutano huo, kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katibu mkuu wizara ya fedha dokta natwe el maamry mwamba amesema uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika katika 1/4 ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025 2026 kwa kufikia 5/100 nukta 8.
Dar es Salaam.
Tanzania imeingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za dunia za utalii WTA kwa mwaka 2025 baada ya kuteuliwa kushiriki katika vipengele 20 vyenye wagombea 24 zikiwemo taasisi na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii.
Akizungumza jijini dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upigaji kura, mkurugenzi wa bodi ya utalii Tanzania ttb ephraim mafuru amesema hatua hiyo ni ya kihistoria inayoonyesha jinsi Tanzania inavyozidi kutambulika kimataifa.
Mafuru amesema tuzo za Tanzania za utalii ni tuzo za kimataifa.
Ambazo zinatambua na kuuthamini ubora ubunifu na huduma bora katika sekta ya utalii na usafiri duniani.
Kwa kumaliza taarifa ya habari sikiliza tena muhtasari wake.
Makamu wa rais, daktari philip mpango amesema Watanzania wana wajibu wa kulinda uhuru wa taifa kuimarisha mshikamano na umoja pamoja na kulinda maadili.
Watanzania wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kushiri.